Zaburi Mlango 130 Psalms

Zaburi 130:1

Ee Bwana, toka vilindini nimekulilia.

Zaburi 130:2

Bwana, uisikie sauti yangu. Masikio yako na yaisikilize Sauti ya dua zangu.

Zaburi 130:3

Bwana, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama?

Zaburi 130:4

Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe.

Zaburi 130:5

Nimemngoja Bwana, roho yangu imengoja, Na neno lake nimelitumainia.

Zaburi 130:6

Nafsi yangu inamngoja Bwana, Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi, Naam, walinzi waingojao asubuhi.

Zaburi 130:7

Ee Israeli, umtarajie Bwana; Maana kwa Bwana kuna fadhili, Na kwake kuna ukombozi mwingi.

Zaburi 130:8

Yeye atamkomboa Israeli na maovu yake yote.