Zaburi Mlango 116 Psalms

Zaburi 116:1

Haleluya. Nampenda Bwana kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu.

Zaburi 116:2

Kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote.

Zaburi 116:3

Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni;

Zaburi 116:4

Nikaliitia jina la Bwana. Ee Bwana, nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu.

Zaburi 116:5

Bwana ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema.

Zaburi 116:6

Bwana huwalinda wasio na hila; Nalidhilika, akaniokoa.

Zaburi 116:7

Ee nafsi yangu, urudi rahani mwako, Kwa kuwa Bwana amekutendea ukarimu.

Zaburi 116:8

Maana umeniponya nafsi yangu na mauti, Macho yangu na machozi, Na miguu yangu na kuanguka.

Zaburi 116:9

Nitaenenda mbele za Bwana Katika nchi za walio hai.

Zaburi 116:10

Naliamini, kwa maana nitasema, Mimi naliteswa sana.

Zaburi 116:11

Mimi nalisema kwa haraka yangu, Wanadamu wote ni waongo.

Zaburi 116:12

Nimrudishie Bwana nini Kwa ukarimu wake wote alionitendea?

Zaburi 116:13

Nitakipokea kikombe cha wokovu; Na kulitangaza jina la Bwana;

Zaburi 116:14

Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana, Naam, mbele ya watu wake wote.

Zaburi 116:15

Ina thamani machoni pa Bwana Mauti ya wacha Mungu wake.

Zaburi 116:16

Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako, Mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako, Umevifungua vifungo vyangu.

Zaburi 116:17

Nitakutolea dhabihu ya kushukuru; Na kulitangaza jina la Bwana;

Zaburi 116:18

Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana, Naam, mbele ya watu wake wote.

Zaburi 116:19

Katika nyua za nyumba ya Bwana, Ndani yako, Ee Yerusalemu.