Zaburi Mlango 32 Psalms

Zaburi 32:1

Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake.

Zaburi 32:2

Heri Bwana asiyemhesabia upotovu, Ambaye rohoni mwake hamna hila.

Zaburi 32:3

Niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa Kwa kuugua kwangu mchana kutwa.

Zaburi 32:4

Kwa maana mchana na usiku Mkono wako ulinilemea. Jasho langu likakauka hata nikawa Kama nchi kavu wakati wa kaskazi.

Zaburi 32:5

Nalikujulisha dhambi yangu, Wala sikuuficha upotovu wangu. Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa Bwana, Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.

Zaburi 32:6

Kwa hiyo kila mtu mtauwa Akuombe wakati unapopatikana. Hakika maji makuu yafurikapo, Hayatamfikia yeye.

Zaburi 32:7

Ndiwe sitara yangu, utanihifadhi na mateso, Utanizungusha nyimbo za wokovu.

Zaburi 32:8

Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.

Zaburi 32:9

Msiwe kama farasi wala nyumbu, Walio hawana akili. Kwa matandiko ya lijamu na hatamu Sharti kuwazuia hao, au hawatakukaribia.

Zaburi 32:10

Naye mtu mwovu ana mapigo mengi, Bali amtumainiye Bwana fadhili zitamzunguka.

Zaburi 32:11

Mfurahieni Bwana; Shangilieni, enyi wenye haki Pigeni vigelegele vya furaha; Ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo.