Zaburi Mlango 14 Psalms

Zaburi 14:1

Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.

Zaburi 14:2

Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.

Zaburi 14:3

Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.

Zaburi 14:4

Je! Wote wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, Hawamwiti Bwana.

Zaburi 14:5

Hapo ndipo walipoingiwa na hofu nyingi, Maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki.

Zaburi 14:6

Mnalitia aibu shauri la mtu mnyonge, Bali Bwana ndiye aliye kimbilio lake.

Zaburi 14:7

Laiti wokovu wa Israeli utoke katika Sayuni! Bwana awarudishapo wafungwa wa watu wake; Yakobo atashangilia, Israeli atafurahi.