Zaburi Mlango 95 Psalms

Zaburi 95:1

Njoni, tumwimbie Bwana, Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.

Zaburi 95:2

Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi.

Zaburi 95:3

Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu, Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.

Zaburi 95:4

Mkononi mwake zimo bonde za dunia, Hata vilele vya milima ni vyake.

Zaburi 95:5

Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya, Na mikono yake iliumba nchi kavu.

Zaburi 95:6

Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba.

Zaburi 95:7

Kwa maana ndiye Mungu wetu, Na sisi tu watu wa malisho yake, Na kondoo za mkono wake. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!

Zaburi 95:8

Msifanye migumu mioyo yenu; Kama vile huko Meriba Kama siku ya Masa jangwani.

Zaburi 95:9

Hapo waliponijaribu baba zenu, Wakanipima, wakayaona matendo yangu.

Zaburi 95:10

Miaka arobaini nalihuzunika na kizazi kile, Nikasema, Hao ni watu waliopotoka mioyo, Hawakuzijua njia zangu.

Zaburi 95:11

Nikaapa kwa hasira yangu Wasiingie rahani mwangu.