Zaburi Mlango 26 Psalms

Zaburi 26:1

Ee Bwana, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini Bwana bila wasiwasi.

Zaburi 26:2

Ee Bwana, unijaribu na kunipima; Unisafishe mtima wangu na moyo wangu.

Zaburi 26:3

Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu, Nami nimekwenda katika kweli yako.

Zaburi 26:4

Sikuketi pamoja na watu wa ubatili, Wala sitaingia mnamo wanafiki.

Zaburi 26:5

Nimelichukia kusanyiko la watenda mabaya, Wala sitaketi pamoja na watu waovu.

Zaburi 26:6

Nitanawa mikono yangu kwa kutokuwa na hatia, Na kuizunguka madhabahu yako, Ee Bwana

Zaburi 26:7

Ili niitangaze sauti ya kushukuru, Na kuzisimulia kazi zako za ajabu.

Zaburi 26:8

Bwana, nimependa makao ya nyumba yako, Na mahali pa maskani ya utukufu wako.

Zaburi 26:9

Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji, Wala uhai wangu pamoja na watu wa damu.

Zaburi 26:10

Mikononi mwao mna madhara, Na mkono wao wa kuume umejaa rushwa.

Zaburi 26:11

Ila mimi nitakwenda kwa ukamilifu wangu; Unikomboe, unifanyie fadhili.

Zaburi 26:12

Mguu wangu umesimama palipo sawa; Katika makusanyiko nitamhimidi Bwana.