Zaburi Mlango 89 Psalms

Zaburi 89:1

Fadhili za Bwana nitaziimba milele; Kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako.

Zaburi 89:2

Maana nimesema, Fadhili zitajengwa milele; Katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako.

Zaburi 89:3

Nimefanya agano na mteule wangu, Nimemuapia Daudi, mtumishi wangu.

Zaburi 89:4

Wazao wako nitawafanya imara milele, Nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele.

Zaburi 89:5

Ee Bwana, mbingu zitayasifu maajabu yako, Uaminifu wako katika kusanyiko la watakatifu.

Zaburi 89:6

Maana ni nani katika mbingu awezaye kulinganishwa na Bwana? Ni nani afananaye na Bwana miongoni mwa malaika?

Zaburi 89:7

Mungu huogopwa sana barazani pa watakatifu, Ni wa kuhofiwa kuliko wote wanaomzunguka.

Zaburi 89:8

Bwana, Mungu wa majeshi, Ni nani aliye hodari kama Wewe, Ee YAHU? Na uaminifu wako unakuzunguka.

Zaburi 89:9

Wewe ndiwe ukitawalaye kiburi cha bahari. Mawimbi yake yainukapo wayatuliza Wewe.

Zaburi 89:10

Ndiwe uliyemseta Rahabu akawa kama aliyeuawa, Kwa mkono hodari umewatawanya wakuchukiao.

Zaburi 89:11

Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako, Ulimwengu na vyote viujazavyo Ndiwe uliyeupiga msingi wake.

Zaburi 89:12

Kaskazini na kusini ndiwe uliyeziumba, Tabori na Hermoni hulifurahia jina lako.

Zaburi 89:13

Mkono wako ni mkono wenye uweza, Mkono wako una nguvu, Mkono wako wa kuume umetukuka.

Zaburi 89:14

Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako, Fadhili na kweli zahudhuria mbele za uso wako.

Zaburi 89:15

Heri watu wale waijuao sauti ya shangwe, Ee Bwana, huenenda katika nuru ya uso wako.

Zaburi 89:16

Kwa jina lako hufurahi mchana kutwa, Na kwa haki yako hutukuzwa.

Zaburi 89:17

Maana fahari ya nguvu zao ni Wewe, Na kwa radhi yako pembe yetu itatukuka.

Zaburi 89:18

Maana ngao yetu ina Bwana, Na mfalme wetu ni wake Mtakatifu wa Israeli.

Zaburi 89:19

Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa njozi, Ukasema, nimempa aliye hodari msaada; Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu.

Zaburi 89:20

Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, Nimempaka mafuta yangu matakatifu.

Zaburi 89:21

Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake, Na mkono wangu utamtia nguvu.

Zaburi 89:22

Adui hatamwonea, Wala mwana wa uovu hatamtesa.

Zaburi 89:23

Bali nitawaponda watesi wake mbele yake, Nitawapiga wanaomchukia.

Zaburi 89:24

Uaminifu wangu na fadhili zangu atakuwa nazo, Na kwa jina langu pembe yake itatukuka.

Zaburi 89:25

Nitaweka mkono wake juu ya bahari, Na mkono wake wa kuume juu ya mito.

Zaburi 89:26

Yeye ataniita, Wewe baba yangu, Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu.

Zaburi 89:27

Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza, Kuwa juu sana kuliko wafalme wa dunia.

Zaburi 89:28

Hata milele nitamwekea fadhili zangu, Na agano langu litafanyika amini kwake.

Zaburi 89:29

Wazao wake nao nitawadumisha milele, Na kiti chake cha enzi kama siku za mbingu.

Zaburi 89:30

Wanawe wakiiacha sheria yangu, Wasiende katika hukumu zangu,

Zaburi 89:31

Wakizihalifu amri zangu, Wasiyashike maagizo yangu,

Zaburi 89:32

Basi, nitawarudi makosa yao kwa fimbo, Na uovu wao kwa mapigo.

Zaburi 89:33

Lakini fadhili zangu sitamwondolea yeye, Wala sitafanya uaminifu wangu kuwa uongo.

Zaburi 89:34

Mimi sitalihalifu agano langu, Sitalibadili neno lililotoka midomoni mwangu.

Zaburi 89:35

Neno moja nimeliapa kwa utakatifu wangu, Hakika sitamwambia Daudi uongo,

Zaburi 89:36

Wazao wake watadumu milele, Na kiti chake kitakuwa kama jua mbele zangu.

Zaburi 89:37

Kitathibitika milele kama mwezi; Shahidi aliye mbinguni mwaminifu.

Zaburi 89:38

Walakini Wewe umemtupa na kumkataa, Umemghadhibikia masihi wako.

Zaburi 89:39

Umechukizwa na agano la mtumishi wako, Umeinajisi taji yake na kuitupa chini.

Zaburi 89:40

Umeyabomoa maboma yake yote, Umezifanya ngome zake kuwa magofu.

Zaburi 89:41

Wote wapitao njiani wanateka mali zake; Amekuwa laumu kwa jirani zake;

Zaburi 89:42

Umeutukuza mkono wa kuume wa watesi wake; Umewafurahisha wote wanaomchukia.

Zaburi 89:43

Pia umeurudisha nyuma ukali wa upanga wake; Wala hukumsimamisha vitani.

Zaburi 89:44

Umeikomesha fahari yake; Kiti chake cha enzi umekitupa chini.

Zaburi 89:45

Umezipunguza siku za ujana wake; Umemvika aibu.

Zaburi 89:46

Ee Bwana, hata lini? Utajificha hata milele? Ghadhabu yako itawaka kama moto?

Zaburi 89:47

Ukumbuke jinsi mimi nisivyo wa kudumu; Kwa ubatili gani umeiumba jamii ya wanadamu!

Zaburi 89:48

Ni mwanamume gani atakayeishi asione mauti, Atakayejiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu?

Zaburi 89:49

Bwana, zi wapi fadhili zako za kwanza, Ulizomwapia Daudi kwa uaminifu wako?

Zaburi 89:50

Ee Bwana, ukumbuke, Wanavyosimangwa watumishi wako; Jinsi ninavyostahimili kifuani mwangu Masimango ya watu wengi.

Zaburi 89:51

Ambayo adui zako wamesimanga, Ee Bwana, Naam, wamezisimanga hatua za masihi wako.

Zaburi 89:52

Na ahimidiwe Bwana milele. Amina na Amina.