Zaburi Mlango 59 Psalms

Zaburi 59:1

Ee Mungu wangu, uniponye na adui zangu, Uniinue juu yao wanaoshindana nami.

Zaburi 59:2

Uniponye nao wafanyao maovu, Uniokoe na watu wa damu.

Zaburi 59:3

Kwa maana wanaiotea nafsi yangu; Wenye nguvu wamenikusanyikia; Ee Bwana, si kwa kosa langu, Wala si kwa hatia yangu.

Zaburi 59:4

Bila kosa langu huenda mbio, hujiweka tayari; Uamke uonane nami, na kutazama.

Zaburi 59:5

Na Wewe, Bwana, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, uamke. Uwapatilize mataifa yote; Usiwarehemu waovu wafanyao uovu hata mmoja.

Zaburi 59:6

Wakati wa jioni hurudi, hulia kama mbwa, Na kuzunguka-zunguka mjini.

Zaburi 59:7

Tazama, kwa vinywa vyao huteuka, Midomoni mwao mna panga, Kwa maana ni nani asikiaye?

Zaburi 59:8

Na Wewe, Bwana, utawacheka, Utawadhihaki mataifa yote.

Zaburi 59:9

Ee nguvu zangu, nitakungoja Wewe, Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu

Zaburi 59:10

Mungu wa fadhili zangu atanitangulia, Mungu atanijalia kuwatazama adui zangu.

Zaburi 59:11

Usiwaue, watu wangu wasije wakasahau; Uwatawanye kwa uweza wako, Na kuwaangamiza, Ee Bwana, ngao yetu.

Zaburi 59:12

Kwa dhambi ya kinywa chao, Na kwa neno la midomo yao, Wanaswe kwa kiburi chao, Kwa ajili ya kulaani na uongo wasemao.

Zaburi 59:13

Uwakomeshe kwa hasira, Uwakomeshe watoweke, Wajue ya kuwa Mungu atawala katika Yakobo, Na hata miisho ya dunia.

Zaburi 59:14

Wakati wa jioni hurudi, hulia kama mbwa, Na kuzunguka-zunguka mjini.

Zaburi 59:15

Watatanga-tanga hao wakitafuta chakula; Wasiposhiba watakesha usiku kucha.

Zaburi 59:16

Nami nitaziimba nguvu zako asubuhi, Nitaziimba fadhili zako kwa furaha. Kwa kuwa ndiwe uliyekuwa ngome yangu, Na makimbilio siku ya shida yangu.

Zaburi 59:17

Ee nguvu zangu, nitakuimbia kwa furaha, Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu, Mungu wa fadhili zangu.