Zaburi Mlango 101 Psalms

Zaburi 101:1

Rehema na hukumu nitaziimba, Ee Bwana, nitakuimbia zaburi.

Zaburi 101:2

Nitaiangalia njia ya unyofu; Utakuja kwangu lini? Nitakwenda kwa unyofu wa moyo Ndani ya nyumba yangu.

Zaburi 101:3

Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami.

Zaburi 101:4

Moyo wa ukaidi utaondoka kwangu, Lililo ovu sitalijua.

Zaburi 101:5

Amsingiziaye jirani yake kwa siri, Huyo nitamharibu. Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno, Huyo sitavumilia naye.

Zaburi 101:6

Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi, Hao wakae nami. Yeye aendaye katika njia kamilifu, Ndiye atakayenitumikia.

Zaburi 101:7

Hatakaa ndani ya nyumba yangu Mtu atendaye hila. Asemaye uongo hatathibitika Mbele ya macho yangu.

Zaburi 101:8

Asubuhi hata asubuhi nitawaharibu Wabaya wote wa nchi. Niwatenge wote watendao uovu Na mji wa Bwana.