Zaburi Mlango 38 Psalms

Zaburi 38:1

Ee Bwana, usinilaumu katika ghadhabu yako, Wala usiniadhibu kwa ukali wa hasira yako.

Zaburi 38:2

Kwa maana mishale yako imenichoma, Na mkono wako umenipata.

Zaburi 38:3

Hamna uzima katika mwili wangu Kwa sababu ya ghadhabu yako. Wala hamna amani mifupani mwangu Kwa sababu ya hatia zangu.

Zaburi 38:4

Maana dhambi zangu zimenifunikiza kichwa, Kama mzigo mzito zimenilemea mno.

Zaburi 38:5

Jeraha zangu zinanuka, zimeoza, Kwa sababu ya upumbavu wangu.

Zaburi 38:6

Nimepindika na kuinama sana, Mchana kutwa nimekwenda nikihuzunika.

Zaburi 38:7

Maana viuno vyangu vimejaa homa, Wala hamna uzima katika mwili wangu.

Zaburi 38:8

Nimedhoofika na kuchubuka sana, Nimeugua kwa fadhaa ya moyo wangu.

Zaburi 38:9

Bwana, haja zangu zote ziko mbele zako, Kuugua kwangu hakukusitirika kwako.

Zaburi 38:10

Moyo wangu unapwita-pwita, Nguvu zangu zimeniacha; Nuru ya macho yangu nayo imeniondoka.

Zaburi 38:11

Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu; Naam, karibu zangu wamesimama mbali.

Zaburi 38:12

Nao wanaoutafuta uhai wangu hutega mitego; Nao wanaotaka kunidhuru hunena mabaya; Na kufikiri hila mchana kutwa.

Zaburi 38:13

Lakini kama kiziwi sisikii, Nami ni kama bubu asiyefumbua kinywa chake.

Zaburi 38:14

Naam, nimekuwa kama mtu asiyesikia, Ambaye hamna hoja kinywani mwake.

Zaburi 38:15

Kwa kuwa nakungoja Wewe, Bwana, Wewe utajibu, Ee Bwana, Mungu wangu.

Zaburi 38:16

Maana nalisema, Wasije wakanifurahia; Mguu wangu ukiteleza wajitukuza juu yangu.

Zaburi 38:17

Kwa maana mimi ni karibu na kusita, Na maumivu yangu yako mbele yangu daima.

Zaburi 38:18

Kwa maana nitaungama uovu wangu, Na kusikitika kwa dhambi zangu.

Zaburi 38:19

Lakini adui zangu ni wazima wenye nguvu, Nao wanaonichukia bure wamekuwa wengi.

Zaburi 38:20

Naam, wakilipa mabaya kwa mema, Huwa adui zangu kwa kuwa nalifuata lililo jema.

Zaburi 38:21

Wewe, Bwana, usiniache, Mungu wangu, usijitenge nami.

Zaburi 38:22

Ufanye haraka kunisaidia, Ee Bwana, wokovu wangu.