Zaburi Mlango 93 Psalms

Zaburi 93:1

Bwana ametamalaki, amejivika adhama, Bwana amejivika, na kujikaza nguvu. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;

Zaburi 93:2

Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani; Wewe ndiwe uliye tangu milele.

Zaburi 93:3

Ee Bwana, mito imepaza, Mito imepaza sauti zake, Mito imepaza uvumi wake.

Zaburi 93:4

Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu, Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo, Bwana Aliye juu ndiye mwenye ukuu.

Zaburi 93:5

Shuhuda zako ni amini sana; Utakatifu ndio uifaao nyumba yako, Ee Bwana, milele na milele.