Zaburi Mlango 60 Psalms

Zaburi 60:1

Ee Mungu, umetutupa na kututawanya, Umekuwa na hasira, uturudishe tena.

Zaburi 60:2

Umeitetemesha nchi na kuipasua, Upaponye palipobomoka, maana inatikisika.

Zaburi 60:3

Umewaonyesha watu wako mazito, Na kutunywesha mvinyo ya kutuyumbisha.

Zaburi 60:4

Umewapa wakuogopao bendera, Ili itwekwe kwa ajili ya kweli.

Zaburi 60:5

Ili wapenzi wako waopolewe, Uokoe kwa mkono wako wa kuume, utuitikie.

Zaburi 60:6

Mungu amenena kwa utakatifu wake, Nami nitashangilia. Nitaigawanya Shekemu, Nitalipima bonde la Sukothi.

Zaburi 60:7

Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu, Na Efraimu ni nguvu ya kichwa changu. Yuda ni fimbo yangu ya kifalme,

Zaburi 60:8

Moabu ni bakuli langu la kunawia. Nitamtupia Edomu kiatu changu, Na kumpigia Filisti kelele za vita.

Zaburi 60:9

Ni nani atakayenipeleka hata mji wenye boma? Ni nani atakayeniongoza hata Edomu?

Zaburi 60:10

Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa? Wala, Ee Mungu, hutoki na majeshi yetu?

Zaburi 60:11

Utuletee msaada juu ya mtesi, Maana wokovu wa binadamu haufai.

Zaburi 60:12

Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.