Zaburi Mlango 2 Psalms

Zaburi 2:1

Mbona mataifa wanafanya ghasia, Na makabila wanatafakari ubatili?

Zaburi 2:2

Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya Bwana, Na juu ya masihi wake.

Zaburi 2:3

Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupia mbali nasi kamba zao.

Zaburi 2:4

Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka.

Zaburi 2:5

Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake, Na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake.

Zaburi 2:6

Nami nimemweka mfalme wangu Juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.

Zaburi 2:7

Nitaihubiri amri; Bwana aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.

Zaburi 2:8

Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako.

Zaburi 2:9

Utawaponda kwa fimbo ya chuma, Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.

Zaburi 2:10

Na sasa, enyi wafalme, fanyeni akili, Enyi waamuzi wa dunia, mwadibiwe.

Zaburi 2:11

Mtumikieni Bwana kwa kicho, Shangilieni kwa kutetemeka.

Zaburi 2:12

Shikeni yaliyo bora asije akafanya hasira, Nanyi mkapotea njiani,Kwa kuwa hasira yake itawaka upesi,Heri wote wanaomkimbilia.