Zaburi Mlango 115 Psalms

Zaburi 115:1

Ee Bwana, kutukuza usitutukuze sisi, Bali ulitukuze jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako, Kwa ajili ya uaminifu wako.

Zaburi 115:2

Kwa nini mataifa kusema, Yuko wapi Mungu wao?

Zaburi 115:3

Lakini Mungu wetu yuko mbinguni, Alitakalo lote amelitenda.

Zaburi 115:4

Sanamu zao ni fedha na dhahabu, Kazi ya mikono ya wanadamu.

Zaburi 115:5

Zina vinywa lakini hazisemi, Zina macho lakini hazioni,

Zaburi 115:6

Zina masikio lakini hazisikii, Zina pua lakini hazisikii harufu,

Zaburi 115:7

Mikono lakini hazishiki, miguu lakini haziendi, Wala hazitoi sauti kwa koo zake.

Zaburi 115:8

Wazifanyao watafanana nazo, Kila mmoja anayezitumainia.

Zaburi 115:9

Enyi Israeli, mtumainini Bwana; Yeye ni msaada wao na ngao yao.

Zaburi 115:10

Enyi mlango wa Haruni, mtumainini Bwana; Yeye ni msaada wao na ngao yao.

Zaburi 115:11

Enyi mmchao Bwana, mtumainini Bwana; Yeye ni msaada wao na ngao yao.

Zaburi 115:12

Bwana ametukumbuka, Naye atatubariki sisi. Ataubariki mlango wa Israeli, Ataubariki mlango wa Haruni,

Zaburi 115:13

Atawabariki wamchao Bwana, Wadogo kwa wakubwa.

Zaburi 115:14

Bwana na awaongeze ninyi, Ninyi na watoto wenu.

Zaburi 115:15

Na mbarikiwe ninyi na Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.

Zaburi 115:16

Mbingu ni mbingu za Bwana, Bali nchi amewapa wanadamu.

Zaburi 115:17

Sio wafu wamsifuo Bwana, Wala wo wote washukao kwenye kimya;

Zaburi 115:18

Bali sisi tutamhimidi Bwana, Tangu leo na hata milele.