Zaburi Mlango 132 Psalms

Zaburi 132:1

Bwana, umkumbukie Daudi Taabu zake zote alizotaabika.

Zaburi 132:2

Ndiye aliyemwapia Bwana, Akaweka nadhiri kwa Shujaa wa Yakobo.

Zaburi 132:3

Sitaingia hemani mwa nyumba yangu, Wala sitapanda matandiko ya kitanda changu;

Zaburi 132:4

Sitaacha macho yangu kuwa na usingizi, Wala kope zangu kusinzia;

Zaburi 132:5

Hata nitakapompatia Bwana mahali, Na Shujaa wa Yakobo maskani.

Zaburi 132:6

Tazama, tulisikia habari zake katika Efrata, Katika konde la Yearimu tuliiona.

Zaburi 132:7

Na tuingie katika maskani yake, Tusujudu penye kiti cha kuwekea miguu yake.

Zaburi 132:8

Ee Bwana, uinuke, uende kwenye raha yako, Wewe na sanduku la nguvu zako.

Zaburi 132:9

Makuhani wako na wavikwe haki, Watauwa wako na washangilie.

Zaburi 132:10

Kwa ajili ya Daudi, mtumishi wako, Usiurudishe nyuma uso wa masihi

Zaburi 132:11

Bwana amemwapia Daudi neno la kweli, Hatarudi nyuma akalihalifu, Baadhi ya wazao wa mwili wako Nitawaweka katika kiti chako cha enzi.

Zaburi 132:12

Wanao wakiyashika maagano yangu, Na shuhuda nitakazowafundisha; Watoto wao nao wataketi Katika kiti chako cha enzi milele.

Zaburi 132:13

Kwa kuwa Bwana ameichagua Sayuni, Ameitamani akae ndani yake.

Zaburi 132:14

Hapo ndipo mahali pangu pa raha milele, Hapo nitakaa kwa maana nimepatamani.

Zaburi 132:15

Hakika nitavibariki vyakula vyake Wahitaji wake nitawashibisha chakula.

Zaburi 132:16

Na makuhani wake nitawavika wokovu, Na watauwa wake watashangilia.

Zaburi 132:17

Hapo nitamchipushia Daudi pembe, Na taa nimemtengenezea masihi wangu.

Zaburi 132:18

Adui zake nitawavika aibu, Bali juu yake taji yake itasitawi.