Zaburi Mlango 109 Psalms

Zaburi 109:1

Ee Mungu wa sifa zangu, usinyamaze,

Zaburi 109:2

Kwa maana wamenifumbulia kinywa; Kinywa cha mtu asiye haki, cha hila, Wamesema nami kwa ulimi wa uongo.

Zaburi 109:3

Naam, kwa maneno ya chuki wamenizunguka, Wamepigana nami bure.

Zaburi 109:4

Badala ya upendo wangu wao hunishitaki, Ijapokuwa naliwaombea.

Zaburi 109:5

Wamenichukuza mabaya badala ya mema, Na chuki badala ya upendo wangu.

Zaburi 109:6

Uweke mtu mkorofi juu yake, Mshitaki asimame mkono wake wa kuume.

Zaburi 109:7

Katika kuhukumiwa ataonekana hana haki, Na sala yake itadhaniwa kuwa ni dhambi.

Zaburi 109:8

Siku zake na ziwe chache, Usimamizi wake na atwae mtu mwingine.

Zaburi 109:9

Wanawe na wawe yatima, Na mkewe na awe mjane.

Zaburi 109:10

Kutanga na watange wanawe na kuomba, Watafute chakula mbali na mahame yao.

Zaburi 109:11

Mdai na anase vitu vyote alivyo navyo, Wageni na wateke mapato ya kazi yake.

Zaburi 109:12

Asiwe na mtu wa kumfanyia fadhili, Wala mtu wa kuwahurumia yatima wake.

Zaburi 109:13

Wazao wake waangamizwe, Jina lao likafutwe katika kizazi cha pili.

Zaburi 109:14

Uovu wa baba zake ukumbukwe mbele za Bwana, Na dhambi ya mamaye isifutwe.

Zaburi 109:15

Ziwe mbele za Bwana daima, Aliondoe kumbukumbu lao duniani.

Zaburi 109:16

Kwa kuwa hakukumbuka kutenda fadhili, Bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, Hata akamfisha mtu aliyevunjika moyo,

Zaburi 109:17

Naye alipenda kulaani, nako kukampata. Hakupendezwa na kubariki, kukawa mbali naye,

Zaburi 109:18

Alijivika laana kana kwamba ni vazi lake. Ikamwingilia moyoni kama maji, Na kama mafuta mifupani mwake.

Zaburi 109:19

Na iwe kwake kama vazi ajivikalo, Na kama mshipi ajifungao daima.

Zaburi 109:20

Ndiyo malipo ya washitaki wangu toka kwa Bwana, Na ya hao wanaoisingizia nafsi yangu mabaya.

Zaburi 109:21

Na Wewe, MUNGU, Bwana, unitendee kwa ajili ya jina lako, Kwa kuwa fadhili zako ni njema uniokoe.

Zaburi 109:22

Kwa maana mimi ni mnyonge na mhitaji, Na moyo wangu umejeruhi ndani yangu.

Zaburi 109:23

Ninapita kama kivuli kianzacho kutoweka, Ninapeperushwa kama nzige.

Zaburi 109:24

Magoti yangu yamedhoofu kwa kufunga, Na mwili wangu umekonda kwa kukosa mafuta.

Zaburi 109:25

Nami nalikuwa laumu kwao, Wanionapo hutikisa vichwa vyao.

Zaburi 109:26

Ee Bwana, Mungu wangu, unisaidie, Uniokoe sawasawa na fadhili zako.

Zaburi 109:27

Nao wakajue ya kuwa ndio mkono wako; Wewe, Bwana, umeyafanya hayo.

Zaburi 109:28

Wao walaani, bali Wewe utabariki, Wameondoka wao wakaaibishwa, Bali mtumishi wako atafurahi.

Zaburi 109:29

Washitaki wangu watavikwa fedheha, Watajivika aibu yao kama joho.

Zaburi 109:30

Nitamshukuru Bwana kwa kinywa changu, Naam, nitamsifu katikati ya mkutano.

Zaburi 109:31

Maana atasimama mkono wa kuume wa mhitaji Amwokoe na wanaoihukumu nafsi yake.