Zaburi Mlango 3 Psalms

Zaburi 3:1

Bwana, watesi wangu wamezidi kuwa wengi, Ni wengi wanaonishambulia,

Zaburi 3:2

Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu, Hana wokovu huyu kwa Mungu.

Zaburi 3:3

Na Wewe, Bwana, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.

Zaburi 3:4

Kwa sauti yangu namwita Bwana Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.

Zaburi 3:5

Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, Kwa kuwa Bwana ananitegemeza.

Zaburi 3:6

Sitayaogopa makumi elfu ya watu, Waliojipanga juu yangu pande zote.

Zaburi 3:7

Bwana, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki.

Zaburi 3:8

Wokovu una Bwana; Baraka yako na iwe juu ya watu wako.