Zaburi Mlango 97 Psalms

Zaburi 97:1

Bwana ametamalaki, nchi na ishangilie, Visiwa vingi na vifurahi.

Zaburi 97:2

Mawingu na giza vyamzunguka, Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake.

Zaburi 97:3

Moto hutangulia mbele zake, Nao huwateketeza watesi wake pande zote.

Zaburi 97:4

Umeme wake uliuangaza ulimwengu, Nchi ikaona ikatetemeka.

Zaburi 97:5

Milima iliyeyuka kama nta mbele za Bwana, Mbele za Bwana wa dunia yote.

Zaburi 97:6

Mbingu zimetangaza haki yake, Na watu wote wameuona utukufu wake.

Zaburi 97:7

Na waaibishwe wote waabuduo sanamu, Wajivunao kwa vitu visivyofaa; Enyi miungu yote, msujuduni Yeye.

Zaburi 97:8

Sayuni imesikia na kufurahi, Binti za Yuda walishangilia, Kwa sababu ya hukumu zako, Ee Bwana.

Zaburi 97:9

Maana Wewe, Bwana, ndiwe Uliye juu, Juu sana kuliko nchi yote; Umetukuka sana juu ya miungu yote.

Zaburi 97:10

Enyi mmpendao Bwana, uchukieni uovu; Huwalinda nafsi zao watauwa wake, Na kuwaokoa na mkono wa wasio haki.

Zaburi 97:11

Nuru imemzukia mwenye haki, Na furaha wanyofu wa moyo.

Zaburi 97:12

Enyi wenye haki, mmfurahieni Bwana, Na kulishukuru jina lake takatifu.