Zaburi Mlango 48 Psalms

Zaburi 48:1

Bwana ndiye aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima wake mtakatifu.

Zaburi 48:2

Kuinuka kwake ni mzuri sana, Ni furaha ya dunia yote. Mlima Sayuni pande za kaskazini, Mji wa Mfalme mkuu.

Zaburi 48:3

Mungu katika majumba yake Amejijulisha kuwa ngome.

Zaburi 48:4

Maana, tazama, wafalme walikusanyika; Walipita wote pamoja.

Zaburi 48:5

Waliona, mara wakashangaa; Wakafadhaika na kukimbia.

Zaburi 48:6

Papo hapo tetemeko liliwashika, Utungu kama wa mwanamke azaaye.

Zaburi 48:7

Kwa upepo wa mashariki Wavunja jahazi za Tarshishi.

Zaburi 48:8

Kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona, Katika mji wa Bwana wa majeshi. Mji wa Mungu wetu; Mungu ataufanya imara hata milele.

Zaburi 48:9

Tumezitafakari fadhili zako, Ee Mungu, Katikati ya hekalu lako.

Zaburi 48:10

Kama lilivyo jina lako, Ee Mungu, Ndivyo na sifa yako hata miisho ya dunia. Mkono wako wa kuume umejaa haki;

Zaburi 48:11

Na ufurahi mlima Sayuni. Binti za Yuda na washangilie Kwa sababu ya hukumu zako.

Zaburi 48:12

Tembeeni katika Sayuni, Uzungukeni mji, Ihesabuni minara yake,

Zaburi 48:13

Tieni moyoni boma zake, Yafikirini majumba yake, Mpate kuwaambia kizazi kitakachokuja.

Zaburi 48:14

Kwa maana ndivyo alivyo MUNGU, Mungu wetu. Milele na milele Yeye ndiye atakayetuongoza.