Zaburi Mlango 143 Psalms

Zaburi 143:1

Ee Bwana, uisikie sala yangu, uzisikilize dua zangu, Kwa uaminifu wako unijibu kwa haki yako.

Zaburi 143:2

Wala usimhukumu mtumishi wako, Maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki.

Zaburi 143:3

Maana adui ameifuatia nafsi yangu, Ameutupa chini uzima wangu. Amenikalisha mahali penye giza, Kama watu waliokufa zamani.

Zaburi 143:4

Na roho yangu imezimia ndani yangu, Moyo wangu ndani yangu umesituka.

Zaburi 143:5

Nimezikumbuka siku za kale, Nimeyatafakari matendo yako yote, Naziwaza kazi za mikono yako.

Zaburi 143:6

Nakunyoshea mikono yangu; Nafsi yangu inakuonea kiu kama nchi kame.

Zaburi 143:7

Ee Bwana, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni

Zaburi 143:8

Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unijulishe njia nitakayoiendea, Kwa maana nakuinulia nafsi yangu.

Zaburi 143:9

Ee Bwana, uniponye na adui zangu; Nimekukimbilia Wewe, unifiche.

Zaburi 143:10

Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa,

Zaburi 143:11

Ee Bwana, unihuishe kwa ajili ya jina lako, Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni;

Zaburi 143:12

Kwa fadhili zako utawakatilia mbali adui zangu; Na kuwaangamiza wote wanitesao nafsi, Kwa maana mimi ni mtumishi wako.