Zaburi Mlango 145 Psalms

Zaburi 145:1

Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi jina lako milele na milele.

Zaburi 145:2

Kila siku nitakuhimidi, Nitalisifu jina lako milele na milele.

Zaburi 145:3

Bwana ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana, Wala ukuu wake hautambulikani.

Zaburi 145:4

Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako, Kitayatangaza matendo yako makuu.

Zaburi 145:5

Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako, Na matendo yako yote ya ajabu.

Zaburi 145:6

Watu watayataja matendo yako ya kutisha, Nami nitausimulia ukuu wako.

Zaburi 145:7

Watalihubiri kumbukumbu la wema wako mkuu. Wataiimba haki yako.

Zaburi 145:8

Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,

Zaburi 145:9

Bwana ni mwema kwa watu wote, Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote.

Zaburi 145:10

Ee Bwana, kazi zako zote zitakushukuru, Na wacha Mungu wako watakuhimidi.

Zaburi 145:11

Wataunena utukufu wa ufalme wako, Na kuuhadithia uweza wako.

Zaburi 145:12

Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu, Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.

Zaburi 145:13

Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote, Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.

Zaburi 145:14

Bwana huwategemeza wote waangukao, Huwainua wote walioinama chini.

Zaburi 145:15

Macho ya watu wote yakuelekea Wewe, Nawe huwapa chakula chao wakati wake.

Zaburi 145:16

Waufumbua mkono wako, Wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake.

Zaburi 145:17

Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote, Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.

Zaburi 145:18

Bwana yu karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu.

Zaburi 145:19

Atawafanyia wamchao matakwa yao, Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.

Zaburi 145:20

Bwana huwahifadhi wote wampendao, Na wote wasio haki atawaangamiza.

Zaburi 145:21

Kinywa changu kitazinena sifa za Bwana; Wote wenye mwili na walihimidi jina lake takatifu milele na milele.