Zaburi Mlango 123 Psalms

Zaburi 123:1

Nimekuinulia macho yangu, Wewe uketiye mbinguni.

Zaburi 123:2

Kama vile macho ya watumishi Kwa mkono wa bwana zao Kama macho ya mjakazi Kwa mkono wa bibi yake; Hivyo macho yetu humwelekea Bwana, Mungu wetu, Hata atakapoturehemu.

Zaburi 123:3

Uturehemu, Ee Bwana, uturehemu sisi, Kwa maana tumeshiba dharau.

Zaburi 123:4

Nafsi zetu zimeshiba mzaha wa wenye raha, Na dharau ya wenye kiburi.