Zaburi Mlango 73 Psalms

Zaburi 73:1

Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, Kwa hao walio safi mioyo yao.

Zaburi 73:2

Nami miguu yangu ilikuwa karibu na kupotoka, Hatua zangu zilikuwa karibu na kuteleza.

Zaburi 73:3

Maana naliwaonea wivu wenye kujivuna, Nilipoiona hali ya amani ya wasio haki.

Zaburi 73:4

Maana hawana maumivu katika kufa kwao, Na mwili wao una nguvu.

Zaburi 73:5

Katika taabu ya watu hawamo, Wala hawapati mapigo pamoja na wanadamu.

Zaburi 73:6

Hivyo kiburi kimekuwa mkufu shingoni mwao, Jeuri huwavika kama nguo.

Zaburi 73:7

Macho yao hutokeza kwa kunenepa, Wameipita kadiri ya mawazo ya mioyo yao.

Zaburi 73:8

Hudhihaki, husimulia mabaya, Husimulia udhalimu kana kwamba wako juu.

Zaburi 73:9

Wameweka kinywa chao mbinguni, Na ulimi wao hutanga-tanga duniani.

Zaburi 73:10

Kwa hiyo watu wake hugeuka huko, Na maji yaliyojaa humezwa nao.

Zaburi 73:11

Nao husema, Mungu ajuaje? Yako maarifa kwake aliye juu?

Zaburi 73:12

Fahamu, ndivyo walivyo wasio haki, Na kwa kustarehe sikuzote wamepata mali nyingi.

Zaburi 73:13

Hakika nimejisafisha moyo wangu bure, Nimenawa mikono yangu kwa kutokukosa.

Zaburi 73:14

Maana mchana kutwa nimepigwa, Na kuadhibiwa kila asubuhi.

Zaburi 73:15

Kama ningalisema, Nitasimulia kama hayo; Kumbe! Ningaliwadanganya kizazi cha wana wako.

Zaburi 73:16

Nami nalifikiri jinsi ya kufahamu hayo; Ikawa taabu machoni pangu;

Zaburi 73:17

Hata nilipoingia katika patakatifu pa Mungu, Nikautafakari mwisho wao.

Zaburi 73:18

Hakika Wewe huwaweka penye utelezi, Huwaangusha mpaka palipoharibika.

Zaburi 73:19

Namna gani wamekuwa ukiwa mara! Wametokomea na kutoweshwa kwa utisho.

Zaburi 73:20

Ee Bwana, kama ndoto wakati wa kuamka, Uondokapo utaidharau sanamu yao.

Zaburi 73:21

Moyo wangu ulipoona uchungu, Viuno vyangu viliponichoma,

Zaburi 73:22

Nalikuwa kama mjinga, sijui neno; Nalikuwa kama mnyama tu mbele zako.

Zaburi 73:23

Walakini mimi ni pamoja nawe daima, Umenishika mkono wa kuume.

Zaburi 73:24

Utaniongoza kwa shauri lako, Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu.

Zaburi 73:25

Ni nani niliye naye mbinguni, Wala duniani sina cha kupendeza ila Wewe.

Zaburi 73:26

Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele.

Zaburi 73:27

Maana wajitengao nawe watapotea; Umewaangamiza wote waliokuacha Wewe.

Zaburi 73:28

Nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu; Nimefanya kimbilio kwa Bwana MUNGU, Niyahubiri matendo yako yote.