Zaburi Mlango 140 Psalms

Zaburi 140:1

Ee Bwana, uniokoe na mtu mbaya, Unihifadhi na mtu wa jeuri.

Zaburi 140:2

Waliowaza mabaya mioyoni mwao, Kila siku huondokesha vita.

Zaburi 140:3

Wamenoa ndimi zao kama nyoka, Sumu ya fira i chini ya midomo yao.

Zaburi 140:4

Ee Bwana, unilinde na mikono ya mtu asiye haki; Unihifadhi na mtu wa jeuri; Waliowaza kuzipotosha hatua zangu.

Zaburi 140:5

Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba; Wametandika wavu kando ya njia; Wameniwekea matanzi.

Zaburi 140:6

Nimemwambia Bwana, Ndiwe Mungu wangu; Ee Bwana, uisikie sauti ya dua zangu.

Zaburi 140:7

Ee MUNGU Bwana, nguvu za wokovu wangu, Umenifunika kichwa changu siku ya vita.

Zaburi 140:8

Ee Bwana, usimpe asiye haki tamaa zake, Usiifanikishe hila yake, wasije wakajiinua.

Zaburi 140:9

Nao wainuapo vichwa watu wanaonizunguka, Madhara ya midomo yao yawafunike.

Zaburi 140:10

Makaa ya moto yawaangukie, watupwe motoni, Na katika mashimo, wasipate kusimama tena.

Zaburi 140:11

Msingiziaji hatawekwa imara katika nchi, Mtu wa jeuri, uovu humwinda kumwangamiza.

Zaburi 140:12

Najua ya kuwa Bwana atamfanyia mnyonge hukumu, Na wahitaji haki yao.

Zaburi 140:13

Hakika wenye haki watalishukuru jina lako, Wenye adili watakaa mahali ulipo Wewe.