Zaburi Mlango 82 Psalms

Zaburi 82:1

Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu; Katikati ya miungu anahukumu.

Zaburi 82:2

Hata lini mtahukumu kwa dhuluma, Na kuzikubali nyuso za wabaya?

Zaburi 82:3

Mfanyieni hukumu maskini na yatima; Mtendeeni haki aliyeonewa na fukara;

Zaburi 82:4

Mwokoeni maskini na mhitaji; Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.

Zaburi 82:5

Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani; Misingi yote ya nchi imetikisika.

Zaburi 82:6

Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia.

Zaburi 82:7

Lakini mtakufa kama wanadamu, Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.

Zaburi 82:8

Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi, Maana Wewe utawarithi mataifa yote.