Zaburi Mlango 91 Psalms

Zaburi 91:1

Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.

Zaburi 91:2

Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.

Zaburi 91:3

Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.

Zaburi 91:4

Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.

Zaburi 91:5

Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,

Zaburi 91:6

Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri,

Zaburi 91:7

Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe.

Zaburi 91:8

Ila kwa macho yako utatazama, Na kuyaona malipo ya wasio haki.

Zaburi 91:9

Kwa kuwa Wewe Bwana ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako.

Zaburi 91:10

Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.

Zaburi 91:11

Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.

Zaburi 91:12

Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

Zaburi 91:13

Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.

Zaburi 91:14

Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.

Zaburi 91:15

Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;

Zaburi 91:16

Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.