Zaburi Mlango 20 Psalms

Zaburi 20:1

Bwana akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue.

Zaburi 20:2

Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni.

Zaburi 20:3

Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako.

Zaburi 20:4

Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote.

Zaburi 20:5

Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. Bwana akutimizie matakwa yako yote.

Zaburi 20:6

Sasa najua kuwa Bwana amwokoa masihi wake;Atamjibu kutoka mbingu zake takatifu.

Zaburi 20:7

Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu.

Zaburi 20:8

Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama.

Zaburi 20:9

Bwana, umwokoe mfalme, Utuitikie siku tuitayo.