Zaburi Mlango 83 Psalms

Zaburi 83:1

Ee Mungu, usistarehe, Ee Mungu, usinyamae, wala usitulie.

Zaburi 83:2

Maana adui zako wanafanya ghasia, Nao wakuchukiao wameviinua vichwa vyao.

Zaburi 83:3

Juu ya watu wako wanafanya hila, Na kushauriana juu yao uliowaficha.

Zaburi 83:4

Wamesema, Njoni, tuwakatilie mbali wasiwe taifa, Na jina la Israeli halitakumbukwa tena.

Zaburi 83:5

Maana wanashauriana kwa moyo mmoja, Juu yako wanafanyana agano.

Zaburi 83:6

Hema za Edomu, na Waishmaeli, Na Moabu, na Wahagari,

Zaburi 83:7

Gebali, na Amoni, na Amaleki, Na Filisti, nao wanaokaa Tiro,

Zaburi 83:8

Ashuri naye amepatana nao, Wamewasaidia wana wa Lutu.

Zaburi 83:9

Uwatende kama Midiani, kama Sisera, Kama Yabini, penye kijito Kishoni.

Zaburi 83:10

Ambao waliangamizwa Endori; Wakawa samadi juu ya nchi.

Zaburi 83:11

Uwafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu, Na masheki yao wote kama Zeba na Zalmuna.

Zaburi 83:12

Ambao Walisema, Na tutamalaki makao ya Mungu.

Zaburi 83:13

Ee Mungu, uwafanye kama mavumbi ya kisulisuli, Mithili ya makapi mbele ya upepo,

Zaburi 83:14

Kama moto uteketezao msitu, Kama miali ya moto iiwashayo milima,

Zaburi 83:15

Ndivyo utakavyowafuatia kwa tufani yako, Na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako.

Zaburi 83:16

Uwajaze nyuso zao fedheha; Wakalitafute jina lako, Bwana.

Zaburi 83:17

Waaibike, wafadhaike milele, Naam, watahayarike na kupotea.

Zaburi 83:18

Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote.