Zaburi Mlango 24 Psalms

Zaburi 24:1

Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake.

Zaburi 24:2

Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha.

Zaburi 24:3

Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?

Zaburi 24:4

Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila.

Zaburi 24:5

Atapokea baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.

Zaburi 24:6

Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.

Zaburi 24:7

Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Inukeni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia.

Zaburi 24:8

Ni nani Mfalme wa utukufu? Bwana mwenye nguvu, hodari, Bwana hodari wa vita.

Zaburi 24:9

Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam, viinueni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia.

Zaburi 24:10

Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? Bwana wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu.