Zaburi Mlango 12 Psalms

Zaburi 12:1

Bwana, uokoe, maana mcha Mungu amekoma, Maana waaminifu wametoweka katika wanadamu.

Zaburi 12:2

Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe, Wenye midomo ya kujipendekeza; Husemezana kwa mioyo ya unafiki;

Zaburi 12:3

Bwana ataikata midomo yote ya kujipendekeza, Nao ulimi unenao maneno ya kiburi;

Zaburi 12:4

Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda; Midomo yetu ni yetu wenyewe, Ni nani aliye bwana juu yetu?

Zaburi 12:5

Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema Bwana, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.

Zaburi 12:6

Maneno ya Bwana ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.

Zaburi 12:7

Wewe, Bwana, ndiwe utakayetuhifadhi, Utatulinda na kizazi hiki milele.

Zaburi 12:8

Wasio haki hutembea pande zote, Ufisadi ukitukuka kati ya wanadamu.