Zaburi Mlango 136 Psalms

Zaburi 136:1

Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:2

Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:3

Mshukuruni Bwana wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:4

Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:5

Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:6

Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:7

Yeye aliyefanya mianga mikubwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:8

Jua litawale mchana; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:9

Mwezi na nyota zitawale usiku; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:10

Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:11

Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:12

Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:13

Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:14

Akawavusha Israeli katikati yake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:15

Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:16

Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:17

Yeye aliyewapiga wafalme wakuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:18

Akawaua wafalme mashuhuri; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:19

Sihoni, mfalme wa Waamori; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:20

Na Ogu, mfalme wa Bashani; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:21

Akaitoa nchi yao iwe urithi; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:22

Urithi wa Israeli mtumishi wake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:23

Aliyetukumbuka katika unyonge wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:24

Akatuokoa na watesi wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:25

Kila chenye mwili akipa chakula chake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zaburi 136:26

Mshukuruni Mungu wa mbingu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.