Zaburi Mlango 21 Psalms

Zaburi 21:1

Ee Bwana, mfalme atazifurahia nguvu zako, Na wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana.

Zaburi 21:2

Umempa haja ya moyo wake, Wala hukumzuilia matakwa ya midomo yake.

Zaburi 21:3

Maana umemsogezea baraka za heri, Umemvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.

Zaburi 21:4

Alikuomba uhai, ukampa, Muda mrefu wa siku nyingi, milele na milele.

Zaburi 21:5

Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako, Heshima na adhama waweka juu yake.

Zaburi 21:6

Maana umemfanya kuwa baraka za milele, Wamfurahisha kwa furaha ya uso wako.

Zaburi 21:7

Kwa kuwa mfalme humtumaini Bwana, Na kwa fadhili zake Aliye juu hataondoshwa.

Zaburi 21:8

Mkono wako utawapata adui zako wote, Mkono wako wa kuume utawapata wanaokuchukia.

Zaburi 21:9

Utawafanya kuwa kama tanuru ya moto, Wakati wa ghadhabu yako. Bwana atawameza kwa ghadhabu yake, Na moto utawala.

Zaburi 21:10

Matunda yao utayaharibu na kuyaondoa katika nchi, Na wazao wao katika wanadamu.

Zaburi 21:11

Madhali walinuia kukutenda mabaya, Waliwaza hila wasipate kuitimiza.

Zaburi 21:12

Kwa maana utawafanya kukupa kisogo, Kwa upote wa uta wako ukiwaelekezea mishale.

Zaburi 21:13

Ee Bwana, utukuzwe kwa nguvu zako, Nasi tutaimba na kuuhimidi uweza wako.