Zaburi Mlango 111 Psalms

Zaburi 111:1

Haleluya Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote,Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.

Zaburi 111:2

Matendo ya Bwana ni makuu, Yafikiriwa sana na wapendezwao nayo.

Zaburi 111:3

Kazi yake ni heshima na adhama, Na haki yake yakaa milele.

Zaburi 111:4

Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu; Bwana ni mwenye fadhili na rehema.

Zaburi 111:5

Amewapa wamchao chakula; Atalikumbuka agano lake milele.

Zaburi 111:6

Amewajulisha watu wake uwezo wa matendo yake, Kwa kuwapa urithi wa mataifa.

Zaburi 111:7

Matendo ya mikono yake ni kweli na hukumu, Maagizo yake yote ni amini,

Zaburi 111:8

Yamethibitika milele na milele, Yamefanywa katika kweli na adili.

Zaburi 111:9

Amewapelekea watu wake ukombozi, Ameamuru agano lake liwe la milele, Jina lake ni takatifu la kuogopwa.

Zaburi 111:10

Kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana akili njema, Sifa zake zakaa milele.