Zaburi Mlango 61 Psalms

Zaburi 61:1

Ee Mungu, ukisikie kilio changu, Uyasikilize maombi yangu.

Zaburi 61:2

Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda.

Zaburi 61:3

Kwa maana ulikuwa kimbilio langu, Ngome yenye nguvu adui asinipate.

Zaburi 61:4

Nitakaa katika hema yako milele, Nitaikimbilia sitara ya mbawa zako

Zaburi 61:5

Maana Wewe, Mungu, umezisikia nadhiri zangu. Umewapa urithi wao waliogopao jina lako.

Zaburi 61:6

Utaziongeza siku za mfalme, Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi.

Zaburi 61:7

Atakaa mbele za Mungu milele, Ziagize fadhili na kweli zimhifadhi.

Zaburi 61:8

Ndivyo nitakavyoliimbia jina lako daima, Ili niondoe nadhiri zangu kila siku.