Zaburi Mlango 54 Psalms

Zaburi 54:1

Ee Mungu, kwa jina lako uniokoe, Na kwa uweza wako unifanyie hukumu.

Zaburi 54:2

Ee Mungu, uyasikie maombi yangu, Uyasikilize maneno ya kinywa changu.

Zaburi 54:3

Kwa maana wageni wamenishambulia; Watu watishao wananitafuta nafsi yangu; Hawakumweka Mungu mbele yao.

Zaburi 54:4

Tazama, Mungu ndiye anayenisaidia; Bwana ndiye anayenitegemeza nafsi yangu.

Zaburi 54:5

Atawarudishia adui zangu ubaya wao; Uwaangamize kwa uaminifu wako.

Zaburi 54:6

Kwa ukunjufu wa moyo nitakutolea dhabihu; Ee Bwana, nitalishukuru jina lako, maana ni jema.

Zaburi 54:7

Kwa kuwa limeniokoa na kila taabu; Na jicho langu limeridhika Kwa kuwatazama adui zangu.