Zaburi Mlango 46 Psalms

Zaburi 46:1

Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

Zaburi 46:2

Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.

Zaburi 46:3

Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.

Zaburi 46:4

Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye juu.

Zaburi 46:5

Mungu yu katikati yake hautatetemeshwa; Mungu atausaidia asubuhi na mapema.

Zaburi 46:6

Mataifa yalighadhibika, falme zikataharuki; Alitoa sauti yake, nchi ikayeyuka.

Zaburi 46:7

Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.

Zaburi 46:8

Njoni myatazame matendo ya Bwana, Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.

Zaburi 46:9

Avikomesha vita hata mwisho wa dunia; Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari.

Zaburi 46:10

Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.

Zaburi 46:11

Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.