Zaburi 72 Swahili & English

Listen/Download Audio
Zaburi 72 (Swahili) Psalms 72 (English)

Ee Mungu, mpe mfalme hukumu zako, Na mwana wa mfalme haki yako. Zaburi 72:1

> God, give the king your justice; Your righteousness to the royal son.

Atawaamua watu wako kwa haki, Na watu wako walioonewa kwa hukumu. Zaburi 72:2

He will judge your people with righteousness, And your poor with justice.

Milima itawazalia watu amani, Na vilima navyo kwa haki. Zaburi 72:3

The mountains shall bring prosperity to the people. The hills bring the fruit of righteousness.

Atawahukumu walioonewa wa watu, Atawaokoa wahitaji, atamseta mwenye kuonea. Zaburi 72:4

He will judge the poor of the people. He will save the children of the needy, And will break the oppressor in pieces.

Watakuogopa wakati wote wa kudumu jua, Na wakati wa kung'aa mwezi kizazi hata kizazi. Zaburi 72:5

They shall fear you while the sun endures; And as long as the moon, throughout all generations.

Atashuka kama mvua juu ya majani yaliyokatwa, Kama manyunyu yainyweshayo nchi. Zaburi 72:6

He will come down like rain on the mown grass, As showers that water the earth.

Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi, Na wingi wa amani hata mwezi utakapokoma. Zaburi 72:7

In his days, the righteous shall flourish, And abundance of peace, until the moon is no more.

Na awe na enzi toka bahari hata bahari, Toka Mto hata miisho ya dunia. Zaburi 72:8

He shall have dominion also from sea to sea, From the River to the ends of the earth.

Wakaao jangwani na wainame mbele zake; Adui zake na warambe mavumbi. Zaburi 72:9

Those who dwell in the wilderness shall bow before him. His enemies shall lick the dust.

Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa. Zaburi 72:10

The kings of Tarshish and of the isles will bring tribute. The kings of Sheba and Seba shall offer gifts.

Naam, wafalme wote na wamsujudie; Na mataifa yote wamtumikie. Zaburi 72:11

Yes, all kings shall fall down before him. All nations shall serve him.

Kwa maana atamkomboa mhitaji aliapo, Na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi. Zaburi 72:12

For he will deliver the needy when he cries; The poor, who has no helper.

Atamhurumia aliye dhaifu na maskini, Na nafsi za wahitaji ataziokoa. Zaburi 72:13

He will have pity on the poor and needy. He will save the souls of the needy.

Atawakomboa nafsi zao na kuonewa na udhalimu, Na damu yao ina thamani machoni pake. Zaburi 72:14

He will redeem their soul from oppression and violence. Their blood will be precious in his sight.

Basi na aishi; Na wampe dhahabu ya Sheba; Na wamwombee daima; Na kumbariki mchana kutwa. Zaburi 72:15

They shall live, and to him shall be given of the gold of Sheba. Men shall pray for him continually. They shall bless him all day long.

Na uwepo wingi wa nafaka Katika ardhi juu ya milima; Matunda yake na yawaye-waye kama Lebanoni, Na watu wa mjini wasitawi kama majani ya nchi. Zaburi 72:16

There shall be abundance of grain throughout the land. Its fruit sways like Lebanon. Let it flourish, thriving like the grass of the field.

Jina lake na lidumu milele, Pindi ling'aapo jua jina lake liwe na wazao; Mataifa yote na wajibariki katika yeye, Na kumwita heri. Zaburi 72:17

His name endures forever. His name continues as long as the sun. Men shall be blessed by him. All nations will call him blessed.

Na ahimidiwe Bwana, Mungu, Mungu wa Israeli, Atendaye miujiza Yeye peke yake; Zaburi 72:18

Praise be to Yahweh God, the God of Israel, Who alone does marvelous deeds.

Jina lake tukufu na lihimidiwe milele; Dunia yote na ijae utukufu wake. Amina na Amina. Zaburi 72:19

Blessed be his glorious name forever! Let the whole earth be filled with his glory! Amen and amen.

Maombi ya Daudi mwana wa Yese yamekwisha. Zaburi 72:20

This ends the prayers by David, the son of Jesse.