Zaburi 68 Swahili & English

Listen/Download Audio
Zaburi 68 (Swahili) Psalms 68 (English)

Mungu huondoka, adui zake wakatawanyika, Nao wamchukiao huukimbia uso wake. Zaburi 68:1

> Let God arise! Let his enemies be scattered! Let them who hate him also flee before him.

Kama moshi upeperushwavyo, Ndivyo uwapeperushavyo wao; Kama nta iyeyukavyo mbele ya moto, Ndivyo waovu wapoteavyo usoni pa Mungu. Zaburi 68:2

As smoke is driven away, So drive them away. As wax melts before the fire, So let the wicked perish at the presence of God.

Bali wenye haki hufurahi, Na kuushangilia uso wa Mungu, Naam, hupiga kelele kwa furaha. Zaburi 68:3

But let the righteous be glad. Let them rejoice before God. Yes, let them rejoice with gladness.

Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake, Mtengenezeeni njia ya barabara, Apitaye majangwani kama mpanda farasi; Jina lake ni YAHU; shangilieni mbele zake. Zaburi 68:4

Sing to God! Sing praises to his name! Extol him who rides on the clouds: To Yah, his name! Rejoice before him!

Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane, Mungu katika kao lake takatifu. Zaburi 68:5

A father of the fatherless, and a defender of the widows, Is God in his holy habitation.

Mungu huwakalisha wapweke nyumbani; Huwatoa wafungwa wakae hali ya kufanikiwa; Bali wakaidi hukaa katika nchi kavu. Zaburi 68:6

God sets the lonely in families. He brings out the prisoners with singing, But the rebellious dwell in a sun-scorched land.

Ee Mungu, ulipotoka mbele ya watu wako, Ulipopita nyikani, Zaburi 68:7

God, when you went forth before your people, When you marched through the wilderness... Selah.

Nchi ilitetemeka Naam, mbingu zilidondoka usoni pa Mungu; Hata Sinai usoni pa Mungu; Mungu wa Israeli. Zaburi 68:8

The earth trembled. The sky also poured down rain at the presence of the God of Sinai-- At the presence of God, the God of Israel.

Ee Mungu, ulinyesha mvua ya neema; Urithi wako ulipochoka uliutia nguvu. Zaburi 68:9

You, God, sent a plentiful rain. You confirmed your inheritance, when it was weary.

Kabila yako ilifanya kao lake huko; Ee Mungu, kwa wema wako uliwaruzuku walioonewa. Zaburi 68:10

Your congregation lived therein. You, God, prepared your goodness for the poor.

Bwana analitoa neno lake; Wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa; Zaburi 68:11

The Lord announced the word. The ones who proclaim it are a great company.

Wafalme wa majeshi wanakimbia, wanakimbia; Na mwanamke akaaye nyumbani agawa nyara. Zaburi 68:12

"Kings of armies flee! They flee!" She who waits at home divides the spoil,

Kwa nini kulala mazizini arukapo hua, Mbawa zake ziking'aa kama fedha Na manyoya yake kama dhahabu? Zaburi 68:13

While you sleep among the campfires, The wings of a dove sheathed with silver, Her feathers with shining gold.

Mwenyezi Mungu alipotawanya wafalme huko, Kulinyesha theluji katika Salmoni. Zaburi 68:14

When the Almighty scattered kings in her, It snowed on Zalmon.

Ni mlima wa Mungu mlima Bashani, Ni mlima mrefu mlima Bashani. Zaburi 68:15

The mountains of Bashan are majestic mountains. The mountains of Bashan are rugged.

Enyi milima mirefu, kwani kuutazama kwa wivu Mlima alioutamani Mungu akae juu yake? Naam, Bwana atakaa juu yake milele. Zaburi 68:16

Why do you look in envy, you rugged mountains, At the mountain where God chooses to reign? Yes, Yahweh will dwell there forever.

Magari ya Mungu ni ishirini elfu, maelfu maelfu; Bwana yumo kati yao kama katika Sinai, Katika patakatifu. Zaburi 68:17

The chariots of God are tens of thousands and thousands of thousands. The Lord is among them, from Sinai, into the sanctuary.

Wewe umepaa juu, umeteka mateka, Umepewa vipawa katikati ya wanadamu; Naam, hata na wakaidi, Bwana Mungu akae nao. Zaburi 68:18

You have ascended on high. You have led away captives. You have received gifts among men, Yes, among the rebellious also, that Yah God might dwell there.

Na ahimidiwe Bwana, Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu; Mungu ndiye wokovu wetu. Zaburi 68:19

Blessed be the Lord, who daily bears our burdens, Even the God who is our salvation. Selah.

Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa; Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana. Zaburi 68:20

God is to us a God of deliverance. To Yahweh, the Lord, belongs escape from death.

Naam, Mungu atakipasua kichwa cha adui zake, Utosi wenye nywele wa mtu afulizaye kukosa. Zaburi 68:21

But God will strike through the head of his enemies, The hairy scalp of such a one as still continues in his guiltiness.

Bwana alisema, Kutoka Bashani nitawarudisha, Nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari; Zaburi 68:22

The Lord said, "I will bring you again from Bashan, I will bring you again from the depths of the sea;

Uuchovye mguu wako katika damu ya adui zako, Na ulimi wa mbwa zako upate sehemu yake. Zaburi 68:23

That you may crush them, dipping your foot in blood, That the tongues of your dogs may have their portion from your enemies."

Ee Mungu, wameiona miendo yako; Miendo ya Mungu wangu, Mfalme wangu, katika patakatifu Zaburi 68:24

They have seen your processions, God, Even the processions of my God, my King, into the sanctuary.

Waimbaji hutangulia, nyuma yao wapigao vinanda, Kati ya wanawali wapiga matari. Zaburi 68:25

The singers went before, the minstrels followed after, In the midst of the ladies playing with tambourines,

Mhimidini Mungu katika mikutano, Bwana katika makusanyiko ya Israeli. Zaburi 68:26

"Bless God in the congregations, Even the Lord in the assembly of Israel!"

Yuko Benyamini mdogo, mtawala wao; Wakuu wa Yuda, kundi lao; Wakuu wa Zabuloni; Wakuu wa Naftali. Zaburi 68:27

There is little Benjamin, their ruler, The princes of Judah, their council, The princes of Zebulun, and the princes of Naphtali.

Ee Mungu, uziamuru nguvu zako; Ee Mungu, uwe hodari uliyetufanyia makuu. Zaburi 68:28

Your God has commanded your strength. Strengthen, God, that which you have done for us.

Kwa ajili ya hekalu lako Yerusalemu Wafalme watakuletea hedaya. Zaburi 68:29

Because of your temple at Jerusalem, Kings shall bring presents to you.

Mkemee mnyama wa manyasini; Kundi la mafahali, na ndama za watu; Hata wanyenyekee na kuleta vipande vya fedha, Uwatawanye watu wapendao vita. Zaburi 68:30

Rebuke the wild animal of the reeds, The multitude of the bulls, with the calves of the peoples. Being humbled, may it bring bars of silver. Scatter the nations that delight in war.

Masheki watakuja kutoka Misri, Kushi itamnyoshea Mungu mikono yake mara. Zaburi 68:31

Princes shall come out of Egypt. Ethiopia shall hurry to stretch out her hands to God.

Enyi falme za dunia, mwimbieni Mungu, Msifuni Bwana kwa nyimbo. Zaburi 68:32

Sing to God, you kingdoms of the earth! Sing praises to the Lord! Selah.

Apandaye mbingu za mbingu za tangu milele; Aitoa sauti yake, sauti ya nguvu. Zaburi 68:33

To him who rides on the heaven of heavens, which are of old; Behold, he utters his voice, a mighty voice.

Mhesabieni Mungu nguvu; Enzi yake i juu ya Israeli; Na nguvu zake zi mawinguni. Zaburi 68:34

Ascribe strength to God! His excellency is over Israel, His strength is in the skies.

Mungu ni mwenye kutisha Kutoka patakatifu pako. Ndiye Mungu wa Israeli; Yeye huwapa watu wake nguvu na uwezo. Na ahimidiwe Mungu. Zaburi 68:35

You are awesome, God, in your sanctuaries. The God of Israel gives strength and power to his people. Praise be to God!