Zaburi 26 Swahili & English

Listen/Download Audio
Zaburi 26 (Swahili) Psalms 26 (English)

Ee Bwana, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini Bwana bila wasiwasi. Zaburi 26:1

> Judge me, Yahweh, for I have walked in my integrity. I have trusted also in Yahweh without wavering.

Ee Bwana, unijaribu na kunipima; Unisafishe mtima wangu na moyo wangu. Zaburi 26:2

Examine me, Yahweh, and prove me. Try my heart and my mind.

Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu, Nami nimekwenda katika kweli yako. Zaburi 26:3

For your loving kindness is before my eyes. I have walked in your truth.

Sikuketi pamoja na watu wa ubatili, Wala sitaingia mnamo wanafiki. Zaburi 26:4

I have not sat with deceitful men, Neither will I go in with hypocrites.

Nimelichukia kusanyiko la watenda mabaya, Wala sitaketi pamoja na watu waovu. Zaburi 26:5

I hate the assembly of evil-doers, And will not sit with the wicked.

Nitanawa mikono yangu kwa kutokuwa na hatia, Na kuizunguka madhabahu yako, Ee Bwana Zaburi 26:6

I will wash my hands in innocence, So I will go about your altar, Yahweh;

Ili niitangaze sauti ya kushukuru, Na kuzisimulia kazi zako za ajabu. Zaburi 26:7

That I may make the voice of thanksgiving to be heard, And tell of all your wondrous works.

Bwana, nimependa makao ya nyumba yako, Na mahali pa maskani ya utukufu wako. Zaburi 26:8

Yahweh, I love the habitation of your house, The place where your glory dwells.

Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji, Wala uhai wangu pamoja na watu wa damu. Zaburi 26:9

Don't gather my soul with sinners, Nor my life with bloodthirsty men;

Mikononi mwao mna madhara, Na mkono wao wa kuume umejaa rushwa. Zaburi 26:10

In whose hands is wickedness, Their right hand is full of bribes.

Ila mimi nitakwenda kwa ukamilifu wangu; Unikomboe, unifanyie fadhili. Zaburi 26:11

But as for me, I will walk in my integrity. Redeem me, and be merciful to me.

Mguu wangu umesimama palipo sawa; Katika makusanyiko nitamhimidi Bwana. Zaburi 26:12

My foot stands in an even place. In the congregations I will bless Yahweh.