Zaburi 10 Swahili & English

Listen/Download Audio
Zaburi 10 (Swahili) Psalms 10 (English)

Ee Bwana, kwa nini wasimama mbali? Kwani kujificha nyakati za shida? Zaburi 10:1

Why do you stand far off, Yahweh? Why do you hide yourself in times of trouble?

Kwa kiburi chake asiye haki mnyonge anafuatiwa kwa ukali; Na wanaswe kwa hila zizo hizo walizoziwaza. Zaburi 10:2

In arrogance, the wicked hunt down the weak; They are caught in the schemes that they devise.

Maana mdhalimu hujisifia tamaa ya nafsi yake, Na mwenye choyo humkana Bwana na kumdharau. Zaburi 10:3

For the wicked boasts of his heart's cravings, He blesses the greedy, and condemns Yahweh.

Mdhalimu kwa kiburi cha uso wake Asema, Hatapatiliza. Jumla ya mawazo yake ni, Hakuna Mungu; Zaburi 10:4

The wicked, in the pride of his face, Has no room in his thoughts for God.

Njia zake ni thabiti kila wakati. Hukumu zako ziko juu asizione, Adui zake wote awafyonya. Zaburi 10:5

His ways are prosperous at all times; He is haughty, and your laws are far from his sight: As for all his adversaries, he sneers at them.

Asema moyoni mwake, Sitaondoshwa, Kizazi baada ya kizazi sitakuwamo taabuni. Zaburi 10:6

He says in his heart, "I shall not be shaken; For generations I shall have no trouble."

Kinywa chake kimejaa laana, Na hila na dhuluma. Chini ya ulimi wake kuna madhara na uovu, Zaburi 10:7

His mouth is full of cursing, deceit, and oppression. Under his tongue is mischief and iniquity.

Hukaa katika maoteo ya vijiji. Mahali pa siri humwua asiye na hatia, Macho yake humvizia mtu duni. Zaburi 10:8

He lies in wait near the villages. From ambushes, he murders the innocent. His eyes are secretly set against the helpless.

Huotea faraghani kama simba pangoni, Huotea amkamate mtu mnyonge. Naam, humkamata mtu mnyonge, Akimkokota wavuni mwake. Zaburi 10:9

He lurks in secret as a lion in his ambush. He lies in wait to catch the helpless. He catches the helpless, when he draws him in his net.

Hujikunyata na kuinama; Watu duni huanguka kwa nguvu zake. Zaburi 10:10

The helpless are crushed, they collapse, They fall under his strength.

Asema moyoni mwake, Mungu amesahau, Auficha uso wake, haoni kamwe. Zaburi 10:11

He says in his heart, "God has forgotten. He hides his face. He will never see it."

Bwana, uondoke, Ee Mungu, uuinue mkono wako, Usiwasahau wanyonge. Zaburi 10:12

Arise, Yahweh! God, lift up your hand! Don't forget the helpless.

Kwani mdhalimu kumdharau Mungu. Akisema moyoni mwake, Hutapatiliza? Zaburi 10:13

Why does the wicked person condemn God, And say in his heart, "God won't call me into account?"

Umeona, maana unaangalia madhara na jeuri, Uyatwae mkononi mwako. Mtu duni hukuachia nafsi yake, Maana umekuwa msaidizi wa yatima. Zaburi 10:14

But you do see trouble and grief; You consider it to take it into your hand. You help the victim and the fatherless.

Uuvunje mkono wake mdhalimu, Na mbaya, uipatilize dhuluma yake, hata usiione. Zaburi 10:15

Break the arm of the wicked. As for the evil man, seek out his wickedness until you find none.

Bwana ndiye Mfalme milele na milele; Mataifa wamepotea kutoka nchi yake. Zaburi 10:16

Yahweh is King forever and ever! The nations will perish out of his land.

Bwana, umeisikia tamaa ya wanyonge, Utaitengeneza mioyo yao, utalitega sikio lako. Zaburi 10:17

Yahweh, you have heard the desire of the humble. You will prepare their heart. You will cause your ear to hear,

Ili kumhukumu yatima naye aliyeonewa, Binadamu aliye udongo asizidi kudhulumu. Zaburi 10:18

To judge the fatherless and the oppressed, That man who is of the earth may terrify no more.