Zaburi 141 Swahili & English

Listen/Download Audio
Zaburi 141 (Swahili) Psalms 141 (English)

Ee Bwana, nimekuita, unijie hima, Uisikie sauti yangu nikuitapo. Zaburi 141:1

> Yahweh, I have called on you. Come to me quickly! Listen to my voice when I call to you.

Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni. Zaburi 141:2

Let my prayer be set before you like incense; The lifting up of my hands like the evening sacrifice.

Ee Bwana, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu. Zaburi 141:3

Set a watch, Yahweh, before my mouth. Keep the door of my lips.

Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya, Nisiyazoelee matendo yasiyofaa, Pamoja na watu watendao maovu; Wala nisile vyakula vyao vya anasa. Zaburi 141:4

Don't incline my heart to any evil thing, To practice deeds of wickedness with men who work iniquity. Don't let me eat of their delicacies.

Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao. Zaburi 141:5

Let the righteous strike me, it is kindness; Let him reprove me, it is like oil on the head; Don't let my head refuse it; Yet my prayer is always against evil deeds.

Makadhi wao wakiangushwa kando ya genge, Watayasikia maneno yangu, maana ni matamu. Zaburi 141:6

Their judges are thrown down by the sides of the rock. They will hear my words, for they are well spoken.

Kama kupasua kuni na kuzichanja juu ya nchi, Ndivyo ilivyo mifupa yetu mdomoni pa kuzimu. Zaburi 141:7

"As when one plows and breaks up the earth, Our bones are scattered at the mouth of Sheol."

Macho yangu yanakuelekea Wewe, MUNGU Bwana, Nimekukimbilia Wewe, usiniache nafsi yangu. Zaburi 141:8

For my eyes are on you, Yahweh, the Lord. In you, I take refuge. Don't leave my soul destitute.

Unilinde na mtego walionitegea, Na matanzi yao watendao maovu. Zaburi 141:9

Keep me from the snare which they have laid for me, From the traps of the workers of iniquity.

Wabaya na waanguke katika nyavu zao wenyewe, Pindi mimi ninapopita salama. Zaburi 141:10

Let the wicked fall together into their own nets, While I pass by.