1 Mambo ya Nyakati Mlango 2 1st Chronicles

1 Mambo ya Nyakati 2:1

Hawa ndio wana wa Israeli; Reubeni, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni;

1 Mambo ya Nyakati 2:2

na Dani, na Yusufu, na Benyamini, na Naftali, na Gadi, na Asheri.

1 Mambo ya Nyakati 2:3

Wana wa Yuda; Eri, na Onani, na Shela; ambao hao watatu alizaliwa na binti Shua, Mkanaani. Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa Bwana; naye akamwua.

1 Mambo ya Nyakati 2:4

Na Tamari, mkwewe, akamzalia Peresi, na Zera. Wana wote wa Yuda ni watano.

1 Mambo ya Nyakati 2:5

Wana wa Peresi; Hesroni, na Hamuli.

1 Mambo ya Nyakati 2:6

Na wana wa Zera; Zabdi, na Ethani, na Hemani, na Kalkoli, na Darda; hao wote ni watano.

1 Mambo ya Nyakati 2:7

Na wana wa Karmi; Akani, yule mwenye kutaabisha Israeli, aliyekosa katika kitu kilichowekwa wakfu.

1 Mambo ya Nyakati 2:8

Na wana wa Ethani; Azaria.

1 Mambo ya Nyakati 2:9

Tena wana wa Hesroni aliozaliwa; Yerameeli, na Ramu, na Kalebu.

1 Mambo ya Nyakati 2:10

Na Ramu akamzaa Aminadabu; na Aminadabu akamzaa Nashoni, mkuu wa wana wa Yuda;

1 Mambo ya Nyakati 2:11

na Nashoni akamzaa Salmoni; na Salmoni akamzaa Boazi;

1 Mambo ya Nyakati 2:12

na Boazi akamzaa Obedi; na Obedi akamzaa Yese;

1 Mambo ya Nyakati 2:13

na Yese akamzaa Eliabu, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Abinadabu, na wa tatu Shama;

1 Mambo ya Nyakati 2:14

na wa nne Nethaneli, na wa tano Radai;

1 Mambo ya Nyakati 2:15

na wa sita Ozemu, na wa saba Daudi;

1 Mambo ya Nyakati 2:16

na maumbu yao ni Seruya, na Abigaili. Na wana wa Seruya walikuwa, Abishai, na Yoabu, na Asaheli; hao watatu.

1 Mambo ya Nyakati 2:17

Na Abigaili akamzaa Amasa; na babaye Amasa ni Yetheri, Mwishmaeli.

1 Mambo ya Nyakati 2:18

Basi Kalebu, mwana wa Hesroni, akazaliwa wana na mkewe Azubu, na Yeriothi, na hawa ndio wanawe wa kiume; Yesheri, na Shobabu, na Ardoni.

1 Mambo ya Nyakati 2:19

Akafa Azuba, naye Kalebu akamtwaa Efrathi, aliyemzalia Huri.

1 Mambo ya Nyakati 2:20

Naye Huri akamzaa Uri; na Uri akamzaa Besaleli.

1 Mambo ya Nyakati 2:21

Na baadaye Hesroni akamwingilia binti wa Makiri, babaye Gileadi; ambaye alimtwaa alipokuwa mwenye miaka sitini; naye akamzalia Segubu.

1 Mambo ya Nyakati 2:22

Na Segubu akamzaa Yairi, aliyekuwa mwenye miji ishirini na mitatu katika nchi ya Gileadi.

1 Mambo ya Nyakati 2:23

Na Geshuri na Aramu wakawapokonya miji ya Yairi, pamoja na Kenathi na miji yake, jumla yote miji sitini. Hao wote ni wana wa Makiri, babaye Gileadi.

1 Mambo ya Nyakati 2:24

Tena, baada ya kufa kwake Hesroni huko Kalebu-Efrata, ndipo Abia, mkewe Hesroni, alipomzalia Ashuri, babaye Teboa.

1 Mambo ya Nyakati 2:25

Na wana wa Yerameeli, mzaliwa wa kwanza wa Hesroni, walikuwa Ramu, mzaliwa wa kwanza, na Buna, na Oreni, na Ozemu; kwa Ahiya.

1 Mambo ya Nyakati 2:26

Naye Yerameeli alikuwa na mke mwingine, jina lake Atara; yeye alikuwa mamaye Onamu.

1 Mambo ya Nyakati 2:27

Na wana wa Ramu, mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli, walikuwa Maasi, na Yamini, na Ekeri.

1 Mambo ya Nyakati 2:28

Na wana wa Onamu walikuwa Shamai, na Yada; na wana wa Shamai; Nadabu, na Abishuri.

1 Mambo ya Nyakati 2:29

Na mkewe Abishuri aliitwa jina lake Abihaili; naye akamzalia Abani, na Molidi.

1 Mambo ya Nyakati 2:30

Na wana wa Nadabu; Seledi, na Apaimu; walakini Seledi alikufa hana watoto.

1 Mambo ya Nyakati 2:31

Na wana wa Apaimu; Ishi. Na wana wa Ishi; Sheshani. Na wana wa Sheshani; Alai.

1 Mambo ya Nyakati 2:32

Na wana wa Yada, nduguye Shamai; Yetheri, na Yonathani; naye Yetheri akafa hana watoto.

1 Mambo ya Nyakati 2:33

Na wana wa Yonathani; Pelethi, na Zaza. Hao ndio wana wa Yerameeli.

1 Mambo ya Nyakati 2:34

Basi huyo Sheshani alikuwa hana wana wa kiume, ila binti. Naye Sheshani alikuwa na mtumwa, Mmisri, jina lake akiitwa Yarha.

1 Mambo ya Nyakati 2:35

Basi akamwoza binti yake aolewe na Yarha, mtumwa wake; naye akamzalia Atai.

1 Mambo ya Nyakati 2:36

Na Atai akamzaa Nathani; na Nathani akamzaa Zabadi;

1 Mambo ya Nyakati 2:37

na Zabadi akamzaa Eflali; na Eflali akamzaa Obedi;

1 Mambo ya Nyakati 2:38

na Obedi akamzaa Yehu; na Yehu akamzaa Azaria;

1 Mambo ya Nyakati 2:39

na Azaria akamzaa Helesi; na Helesi akamzaa Eleasa

1 Mambo ya Nyakati 2:40

na Eleasa akamzaa Sismai; na Sismai akamzaa Shalumu;

1 Mambo ya Nyakati 2:41

na Shalumu akamzaa Yekamia; na Yekamia akamzaa Elishama.

1 Mambo ya Nyakati 2:42

Na wana wa Kalebu, nduguye Yerameeli, walikuwa Mesha, mzaliwa wake wa kwanza, aliyekuwa babaye Zifu; na wana wa Maresha, babaye Hebroni.

1 Mambo ya Nyakati 2:43

Na wana wa Hebroni; Kora, na Tapua, na Rekemu, na Shema.

1 Mambo ya Nyakati 2:44

Naye Shema akamzaa Rahamu, babaye Yorkeamu; na Rekemu akamzaa Shamai.

1 Mambo ya Nyakati 2:45

Na mwana wake Shamai alikuwa Maoni; na Maoni alikuwa babaye Bethsuri.

1 Mambo ya Nyakati 2:46

Naye Efa, suria yake Kalebu, alimzaa Harani, na Mosa, na Gazezi; naye Harani akamzaa Gazezi.

1 Mambo ya Nyakati 2:47

Na wana wa Yadai; Regemu, na Yothamu, na Geshani, na Peleti, na Efa, na Shaafu.

1 Mambo ya Nyakati 2:48

Naye Maaka, suria yake Kalebu, akamzalia Sheberi, na Tirhana.

1 Mambo ya Nyakati 2:49

Tena akamzaa Shaafu, babaye Madmana; na Sheva babaye Makbena; na babaye Gibea; naye binti Kalebu alikuwa Aksa.

1 Mambo ya Nyakati 2:50

Hao walikuwa wana wa Kalebu. Wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi; Shobali, babaye Kiriath-Yearimu;

1 Mambo ya Nyakati 2:51

Salma, babaye Bethlehemu; na Harefu, babaye Beth-gaderi.

1 Mambo ya Nyakati 2:52

Naye Shobali, babaye Kiriath-Yearimu, alikuwa na wana; Haroe, na nusu ya Wamenuhothi.

1 Mambo ya Nyakati 2:53

Na jamaa za Kiriath-Yearimu; Waithri, na Waputhi, na Washumathi, na Wamishrai; katika hao walitoka Wasorathi, na Waeshtaoli.

1 Mambo ya Nyakati 2:54

Na wana wa Salma; Bethlehemu, na Wanetofathi, Atroth-beth-Yoabu, na nusu ya Wamenuhothi, na Wazori.

1 Mambo ya Nyakati 2:55

Na jamaa za waandishi waliokaa Yabesi; Watirathi, na Washimeathi, na Wasukathi. Hao ndio Wakeni, waliotoka kwake Hamathi, babaye mbari ya Rekabu.