1 Mambo ya Nyakati Mlango 25 1st Chronicles

1 Mambo ya Nyakati 25:1

Tena Daudi na maakida wa jeshi wakatenga kwa utumishi baadhi ya wana wa Asafu, na wa Hemani, na wa Yeduthuni, watakaotabiri kwa vinubi na vinanda, na matoazi; hii ndiyo hesabu ya wafanya kazi sawasawa na utumishi wao;

1 Mambo ya Nyakati 25:2

wa wana wa Asafu; Zakuri, na Yusufu, na Nethania, na Asharela, wana wa Asafu; walioamriwa na Asafu, aliyetabiri kwa amri ya mfalme.

1 Mambo ya Nyakati 25:3

Wa Yeduthuni; wana wa Yeduthuni; Gedalia, na Seri, na Yeshaya, na Hashabia, na Matithia, [na Shimei], watu sita; walioamriwa na baba yao Yeduthuni mwenye kinubi, aliyetabiri katika kumshukuru na kumsifu Bwana.

1 Mambo ya Nyakati 25:4

Wa Hemani; wana wa Hemani; Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, na Romanti-ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri, Mahaziothi;

1 Mambo ya Nyakati 25:5

hao wote ndio wana wa Hemani, mwonaji wa mfalme, kwa maneno ya Mungu, ili kuinua pembe. Naye Mungu akampa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu.

1 Mambo ya Nyakati 25:6

Hao wote waliamriwa na baba yao, waimbe nyumbani mwa Bwana, wakiwa na matoazi, vinanda, na vinubi, kwa utumishi wa nyumba ya Mungu; Asafu, Yeduthuni, na Hemani wakiwa wanaamriwa na mfalme.

1 Mambo ya Nyakati 25:7

Na hesabu yao, pamoja na ndugu zao waliofundishwa kumwimbia Bwana, wote waliokuwa wastadi, walikuwa mia mbili na themanini na wanane.

1 Mambo ya Nyakati 25:8

Wakatupiwa kura ya ulinzi wao, sawasawa wote, mdogo kwa mkubwa, mwalimu kwa mwanafunzi.

1 Mambo ya Nyakati 25:9

Kura ya kwanza ikamtokea Yusufu, kwa Asafu; ya pili Gedalia; yeye na nduguze na wanawe, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:10

ya tatu Zakuri, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:11

ya nne Seri, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:12

ya tano Nethania, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:13

ya sita Bukia, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:14

ya saba Asharela, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:15

ya nane Yeshaya, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:16

ya kenda Matania wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:17

ya kumi Shimei, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:18

ya kumi na moja Uzieli, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:19

ya kumi na mbili Hashabia, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:20

ya kumi na tatu Shebueli, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:21

ya kumi na nne Matithia, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:22

ya kumi na tano Yeremothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:23

ya kumi na sita Hanania, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:24

ya kumi na saba Yoshbekasha, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:25

ya kumi na nane Hanani, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:26

ya kumi na kenda Malothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:27

ya ishirini Eliatha, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:28

ya ishirini na moja Hothiri, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:29

ya ishirini na mbili Gidalti, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:30

ya ishirini na tatu Mahaziothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili;

1 Mambo ya Nyakati 25:31

ya ishirini na nne Romanti-ezeri, wanawe na nduguze, kumi na wawili.