1 Mambo ya Nyakati Mlango 9 1st Chronicles

1 Mambo ya Nyakati 9:1

Hivyo Israeli wote walihesabiwa kwa nasaba; na tazama, hizo zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli; na Yuda wakachukuliwa mateka mpaka Babeli, kwa sababu ya makosa yao.

1 Mambo ya Nyakati 9:2

Basi wenyeji wa kwanza waliokaa katika hozi zao katika miji yao walikuwa Israeli, na makuhani, na Walawi, na Wanethini.

1 Mambo ya Nyakati 9:3

Na huko Yerusalemu walikuwa wakikaa baadhi ya wana wa Yuda, na wana wa Benyamini, na wana wa Efraimu na Manase;

1 Mambo ya Nyakati 9:4

Uthai, mwana wa Amihudi, mwana wa Omri, mwana wa Imli, mwana wa Bani, wa wana wa Peresi, mwana wa Yuda.

1 Mambo ya Nyakati 9:5

Na wa Washiloni; Asaya, mzaliwa wa kwanza, na wanawe.

1 Mambo ya Nyakati 9:6

Na wa wana wa Zera; Yeueli, na ndugu zao; watu mia sita na tisini.

1 Mambo ya Nyakati 9:7

Na wa wana wa Benyamini; Salu, mwana wa Meshulamu, mwana wa Hodavia, mwana wa Hasenua;

1 Mambo ya Nyakati 9:8

na Ibneya, mwana wa Yerohamu; na Ela, mwana wa Uzi, mwana wa Mikri; na Meshulamu, mwana wa Shefatia, mwana wa Reueli, mwana wa Ibniya;

1 Mambo ya Nyakati 9:9

na ndugu zao, sawasawa na vizazi vyao; watu mia kenda na hamsini na sita. Watu hao wote ndio waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao, kwa kadiri ya mbari za baba zao.

1 Mambo ya Nyakati 9:10

Na katika makuhani; Yedaya, na Yehoyaribu, na Yakini;

1 Mambo ya Nyakati 9:11

na Azaria, mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu, mkuu wa nyumba ya Mungu;

1 Mambo ya Nyakati 9:12

na Adaya, mwana wa Yerohamu, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya; na Maasai, mwana wa Adieli, mwana wa Yazera, mwana wa Meshulamu, mwana wa Meshilemithi, mwana wa Imeri;

1 Mambo ya Nyakati 9:13

wakuu wa mbari za baba zao; pamoja na ndugu zao; watu elfu na mia saba na sitini; watu wenye ustadi waliofaa sana kwa kazi ya huduma ya nyumba ya Mungu.

1 Mambo ya Nyakati 9:14

Na katika Walawi; Shemaya, mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, wa wana wa Merari;

1 Mambo ya Nyakati 9:15

na Bakbakari, na Hereshi, na Galali, na Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zikri, mwana wa Asafu;

1 Mambo ya Nyakati 9:16

na Obadia, mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni; na Berekia, mwana wa Asa, mwana wa Elkana; waliokaa katika vijiji vya Wanetofathi.

1 Mambo ya Nyakati 9:17

Na katika mabawabu; Shalumu, na Akubu, na Talmoni, na Ahimani, na ndugu zao; naye Shalumu alikuwa mkuu wao;

1 Mambo ya Nyakati 9:18

ambao tangu hapo walikuwa wakingojea penye lango la mfalme upande wa mashariki; hao ndio waliokuwa wangojezi wa rago la wana wa Lawi.

1 Mambo ya Nyakati 9:19

Naye Shalumu, mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora; pamoja na nduguze wa mbari ya babaye, Wakora; walikuwa wakiisimamia kazi hiyo ya huduma, wenye ungojezi wa malango ya maskani; na baba zao walikuwa wamesimamia matuo ya Bwana, wakiyalinda maingilio;

1 Mambo ya Nyakati 9:20

naye Finehasi, mwana wa Eleazari, alikuwa mkuu wao hapo zamani, naye Bwana alikuwa pamoja naye.

1 Mambo ya Nyakati 9:21

Zekaria, mwana wa Meshelemia, alikuwa bawabu mlangoni pa ile hema ya kukutania.

1 Mambo ya Nyakati 9:22

Hao wote waliochaguliwa kuwa wangojezi wa malango walikuwa watu mia mbili na kumi na wawili. Nao wakahesabiwa kwa nasaba katika vijiji vyao, ambao Daudi na Samweli, huyo mwonaji, walikuwa wamewaweka katika kazi yao waliyoamaniwa.

1 Mambo ya Nyakati 9:23

Basi watu hao na wana wao walikuwa na usimamizi wa malango ya nyumba ya Bwana, yaani, nyumba ya maskani, kwa zamu.

1 Mambo ya Nyakati 9:24

Hao wangojezi walikuwapo pande zote nne, kuelekea mashariki, na magharibi, na kaskazini, na kusini.

1 Mambo ya Nyakati 9:25

Na ndugu zao, katika vijiji vyao, wakaamaniwa kuingia kila siku ya saba, zamu kwa zamu, ili kuwa pamoja nao;

1 Mambo ya Nyakati 9:26

kwa maana wale wangojezi wanne, waliokuwa wakuu, nao ni Walawi, walikuwa na kazi ya kuamaniwa, tena walikuwa juu ya vyumba na juu ya hazina katika nyumba ya Mungu.

1 Mambo ya Nyakati 9:27

Nao wakalala kandokando nyumbani mwa Mungu, kwa kuwa ulinzi wake ulikuwa juu yao, nayo ilikuwa kazi yao kuyafungua malango asubuhi baada ya asubuhi.

1 Mambo ya Nyakati 9:28

Na baadhi yao walikuwa na ulinzi wa vyombo vya huduma; kwani huingizwa kwa hesabu, na kutolewa kwa hesabu vile vile.

1 Mambo ya Nyakati 9:29

Na baadhi yao waliamaniwa kuviangalia vyombo vya nyumbani, na vyombo vyote vya Patakatifu; na kuwa juu ya unga safi, na divai, na mafuta, na ubani, na manukato.

1 Mambo ya Nyakati 9:30

Na baadhi ya wana wa makuhani waliweka tayari machanganyiko ya manukato.

1 Mambo ya Nyakati 9:31

Naye Matithia, Mlawi mmojawapo, aliyekuwa mzaliwa wa kwanza wa Shalumu, Mkora, aliamaniwa kazi ya kuviangalia vitu vile vilivyookwa kaangoni.

1 Mambo ya Nyakati 9:32

Na baadhi ya ndugu zao, wa wana wa Wakohathi, walikuwa juu ya mikate ile ya Wonyesho, ili kuiandaa kila sabato.

1 Mambo ya Nyakati 9:33

Tena hawa ndio waimbaji, wakuu wa mbari za baba zao katika Walawi, ambao walikaa vyumbani, kisha walikuwa hawana kazi nyingine; kwa kuwa walitumika katika kazi yao mchana na usiku.

1 Mambo ya Nyakati 9:34

Hao walikuwa wakuu wa mbari za baba zao katika Walawi, katika vizazi vyao vyote, watu wakuu; nao walikuwa wakikaa huko Yerusalemu.

1 Mambo ya Nyakati 9:35

Basi huko Gibea alikaa babaye Gibea, jina lake Yeieli, na jina la mkewe aliitwa Maaka;

1 Mambo ya Nyakati 9:36

na mwanawe, mzaliwa wake wa kwanza, alikuwa Abdoni; na Suri, na Kishi, na Baali, na Meri, na Nadabu;

1 Mambo ya Nyakati 9:37

na Gedori, na Ahio, na Zekaria, na Miklothi.

1 Mambo ya Nyakati 9:38

Na Miklothi akamzaa Shimea. Hao nao walikuwa wakikaa pamoja na ndugu zao huko Yerusalemu, kuwakabili ndugu zao.

1 Mambo ya Nyakati 9:39

Naye Neri akamzaa Kishi; na Kishi akamzaa Sauli; na Sauli akamzaa Yonathani, na Malkishua, na Abinadabu, na Eshbaali.

1 Mambo ya Nyakati 9:40

Na mwana wa Yonathani alikuwa Meribaali; na Meribaali akamzaa Mika.

1 Mambo ya Nyakati 9:41

Na wana wa Mika; Pithoni, na Meleki, na Tarea.

1 Mambo ya Nyakati 9:42

Na Ahazi akamzaa Yara; na Yara akamzaa Alemethi, na Azmawethi, na Zimri; na Zimri akamzaa Mosa;

1 Mambo ya Nyakati 9:43

na Mosa akamzaa Binea; na mwanawe huyo alikuwa Refaya, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli;

1 Mambo ya Nyakati 9:44

naye Aseli alikuwa na wana sita, ambao majina yao ni haya; Azrikamu, na Bokeru, na Ishmaeli, na Shearia, na Obadia, na Hanani. Hao wote walikuwa wana wa Aseli