1 Mambo ya Nyakati 28 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Mambo ya Nyakati 28 (Swahili) 1st Chronicles 28 (English)

Kisha Daudi akawakusanya huko Yerusalemu wakuu wote wa Israeli, wakuu wa kabila, na maakida wa vikosi wenye kumtumikia mfalme kwa zamu, na maakida wa maelfu, na maakida wa mamia, na wenye kutawala juu ya mali na milki za mfalme, na za wanawe, pamoja na matowashi, na mashujaa, naam, waume mashujaa wote. 1 Mambo ya Nyakati 28:1

David assembled all the princes of Israel, the princes of the tribes, and the captains of the companies who served the king by division, and the captains of thousands, and the captains of hundreds, and the rulers over all the substance and possessions of the king and of his sons, with the officers, and the mighty men, even all the mighty men of valor, to Jerusalem.

Ndipo Daudi mfalme akasimama kwa miguu yake, akasema, Nisikilizeni, ndugu zangu, na watu wangu; Mimi nalikuwa na nia ya kuijenga nyumba ya kustarehe kwa ajili ya sanduku la agano la Bwana, na kiti cha kuwekea miguu yake cha Mungu wetu; hata nalikuwa nimeweka tayari kwa kujenga. 1 Mambo ya Nyakati 28:2

Then David the king stood up on his feet, and said, Hear me, my brothers, and my people: as for me, it was in my heart to build a house of rest for the ark of the covenant of Yahweh, and for the footstool of our God; and I had made ready for the building.

Lakini Mungu akaniambia, Wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umekuwa mtu wa vita, nawe umemwaga damu. 1 Mambo ya Nyakati 28:3

But God said to me, You shall not build a house for my name, because you are a man of war, and have shed blood.

Walakini Bwana, Mungu wa Israeli, alinichagua katika nyumba yote ya babangu kuwa mfalme juu ya Israeli milele, kwa kuwa amemchagua Yuda awe mkuu; na katika nyumba ya Yuda, alichagua nyumba ya babangu, na miongoni mwa wana wa babangu, aliniridhia mimi ili kunitawaza niwe mfalme juu ya Israeli wote; 1 Mambo ya Nyakati 28:4

However Yahweh, the God of Israel, chose me out of all the house of my father to be king over Israel forever: for he has chosen Judah to be prince; and in the house of Judah, the house of my father; and among the sons of my father he took pleasure in me to make me king over all Israel;

tena katika wana wangu wote (kwani Bwana amenipa wana wengi), amemchagua Sulemani mwanangu ili aketi juu ya kiti cha enzi cha ufalme wa Bwana, juu ya Israeli. 1 Mambo ya Nyakati 28:5

Of all my sons (for Yahweh has given me many sons), he has chosen Solomon my son to sit on the throne of the kingdom of Yahweh over Israel.

Akaniambia, Sulemani, mwanao, ndiye atakayeijenga nyumba yangu na nyua zangu; kwa kuwa nimemchagua awe mwanangu, nami nitakuwa babaye. 1 Mambo ya Nyakati 28:6

He said to me, Solomon your son, he shall build my house and my courts; for I have chosen him to be my son, and I will be his father.

Na ufalme wake nitauweka imara milele, akijitia kwa bidii kuzitenda amri zangu na hukumu zangu, kama hivi leo. 1 Mambo ya Nyakati 28:7

I will establish his kingdom forever, if he be constant to do my commandments and my ordinances, as at this day.

Basi sasa, machoni pa Israeli wote, hilo kusanyiko la Bwana, na masikioni pa Mungu wetu, angalieni na kuzitafuta amri zote za Bwana, Mungu wenu, ili mpate kuimiliki nchi hii njema, na kuwarithisha wana wenu baada yenu hata milele. 1 Mambo ya Nyakati 28:8

Now therefore, in the sight of all Israel, the assembly of Yahweh, and in the audience of our God, observe and seek out all the commandments of Yahweh your God; that you may possess this good land, and leave it for an inheritance to your children after you forever.

Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa Bwana hutafuta-tafuta mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, ataonekana nawe; ukimwacha, atakutupa milele. 1 Mambo ya Nyakati 28:9

You, Solomon my son, know the God of your father, and serve him with a perfect heart and with a willing mind; for Yahweh searches all hearts, and understands all the imaginations of the thoughts: if you seek him, he will be found of you; but if you forsake him, he will cast you off forever.

Jihadhari basi; kwani Bwana amekuchagua wewe ili ujenge nyumba itakayokuwa mahali patakatifu; uwe hodari ukatende hivyo. 1 Mambo ya Nyakati 28:10

Take heed now; for Yahweh has chosen you to build a house for the sanctuary: be strong, and do it.

Ndipo Daudi akampa Sulemani mwanawe mfano wa ukumbi wa hekalu, na nyumba zake, na hazina zake, na orofa zake, na vyumba vyake vya ndani, na mahali pa kiti cha rehema; 1 Mambo ya Nyakati 28:11

Then David gave to Solomon his son the pattern of the porch [of the temple], and of the houses of it, and of the treasuries of it, and of the upper rooms of it, and of the inner chambers of it, and of the place of the mercy seat;

na mfano wa yote aliyokuwa nayo kwa roho, katika habari ya nyua za nyumba ya Bwana, na ya vyumba vyote vilivyoizunguka, ya hazina za nyumba ya Mungu, na ya hazina za vitu vilivyowekwa wakfu; 1 Mambo ya Nyakati 28:12

and the pattern of all that he had by the Spirit, for the courts of the house of Yahweh, and for all the surrounding rooms, for the treasuries of the house of God, and for the treasuries of the dedicated things;

tena katika habari ya zamu za makuhani na Walawi, na ya kazi yote ya huo utumishi wa nyumba ya Bwana, na ya vyombo vyote vya utumishi nyumbani mwa Bwana; 1 Mambo ya Nyakati 28:13

also for the divisions of the priests and the Levites, and for all the work of the service of the house of Yahweh, and for all the vessels of service in the house of Yahweh;

ya dhahabu kwa uzani kwa vyombo vya dhahabu, kwa vyombo vyote vya utumishi wa kila namna; ya fedha kwa uzani kwa vyombo vyote vya fedha, kwa vyombo vyote vya utumishi wa kila namna; 1 Mambo ya Nyakati 28:14

of gold by weight for the [vessels of] gold, for all vessels of every kind of service; [of silver] for all the vessels of silver by weight, for all vessels of every kind of service;

kwa uzani tena kwa vinara vya dhahabu, na kwa taa zake za dhahabu, kwa uzani, kwa kila kinara, na kwa taa zake; na kwa vinara vya fedha, kwa uzani kwa kila kinara na kwa taa zake, kwa kadiri ya matumizi ya kila kinara; 1 Mambo ya Nyakati 28:15

by weight also for the lampstands of gold, and for the lamps of it, of gold, by weight for every lampstand and for the lamps of it; and for the lampstands of silver, [silver] by weight for [every] lampstand and for the lamps of it, according to the use of every lampstand;

na dhahabu kwa uzani kwa meza za mikate ya wonyesho, kwa kila meza; na fedha kwa meza za fedha; 1 Mambo ya Nyakati 28:16

and the gold by weight for the tables of show bread, for every table; and silver for the tables of silver;

na nyuma, na mabakuli, na vikombe vya dhahabu safi; na kwa matasa ya dhahabu, kwa uzani kwa kila tasa; na kwa matasa ya fedha, kwa uzani kwa kila tasa; 1 Mambo ya Nyakati 28:17

and the flesh-hooks, and the basins, and the cups, of pure gold; and for the golden bowls by weight for every bowl; and for the silver bowls by weight for every bowl;

na kwa madhabahu ya kufukizia, dhahabu iliyosafika sana kwa uzani; na dhahabu kwa mfano wa gari, yaani, makerubi, yenye kutandaza mabawa, na kulifunika sanduku la agano la Bwana. 1 Mambo ya Nyakati 28:18

and for the altar of incense refined gold by weight; and gold for the pattern of the chariot, [even] the cherubim, that spread out [their wings], and covered the ark of the covenant of Yahweh.

Hayo yote, akasema Daudi, yamenielea kwa maandiko kutoka kwa mkono wa Bwana, naam, kazi zote za mfano huu. 1 Mambo ya Nyakati 28:19

All this, [said David], have I been made to understand in writing from the hand of Yahweh, even all the works of this pattern.

Kisha Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Uwe hodari, mwenye moyo mkuu, ukatende hivyo; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu, Mungu wangu, yu pamoja nawe; yeye hatakupungukia wala kukuacha, hata itakapomalizika kazi yote ya huo utumishi wa nyumba ya Bwana. 1 Mambo ya Nyakati 28:20

David said to Solomon his son, Be strong and of good courage, and do it: don't be afraid, nor be dismayed; for Yahweh God, even my God, is with you; he will not fail you, nor forsake you, until all the work for the service of the house of Yahweh is finished.

Na tazama, hizo zamu za makuhani na Walawi ziko, kwa utumishi wote wa nyumba ya Mungu; nao watakuwapo pamoja nawe kwa kazi ya kila namna, kila mtu mwenye hiari, aliye stadi kwa utumishi wo wote; tena maakida na watu wote watakuwa chini ya amri yako kabisa. 1 Mambo ya Nyakati 28:21

Behold, there are the divisions of the priests and the Levites, for all the service of the house of God: and there shall be with you in all manner of work every willing man who has skill, for any manner of service: also the captains and all the people will be entirely at your command.