1 Mambo ya Nyakati Mlango 6 1st Chronicles

1 Mambo ya Nyakati 6:1

Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari.

1 Mambo ya Nyakati 6:2

Na wana wa Kohathi; Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli.

1 Mambo ya Nyakati 6:3

Na wana wa Amramu; Haruni, na Musa, na Miriamu. Na wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.

1 Mambo ya Nyakati 6:4

Eleazari akamzaa Finehasi; na Finehasi akamzaa Abishua;

1 Mambo ya Nyakati 6:5

na Abishua akamzaa Buki; na Buki akamzaa Uzi;

1 Mambo ya Nyakati 6:6

na Uzi akamzaa Zerahia; na Zerahia akamzaa Merayothi,

1 Mambo ya Nyakati 6:7

na Merayothi akamzaa Amaria; na Amaria akamzaa Ahitubu;

1 Mambo ya Nyakati 6:8

na Ahitubu akamzaa Sadoki; na Sadoki akamzaa Ahimaasi;

1 Mambo ya Nyakati 6:9

na Ahimaasi akamzaa Azaria; na Azaria akamzaa Yohana;

1 Mambo ya Nyakati 6:10

na Yohana akamzaa Azaria (ndiye huyo aliyefanya kazi ya ukuhani katika nyumba aliyoijenga Sulemani huko Yerusalemu)

1 Mambo ya Nyakati 6:11

na Azaria akamzaa Amaria; na Amaria akamzaa Ahitubu;

1 Mambo ya Nyakati 6:12

na Ahitubu akamzaa Sadoki; na Sadoki akamzaa Meshulamu;

1 Mambo ya Nyakati 6:13

na Meshulamu akamzaa Hilkia; na Hilkia akamzaa Azaria;

1 Mambo ya Nyakati 6:14

na Azaria akamzaa Seraya; na Seraya akamzaa Yehosadaki;

1 Mambo ya Nyakati 6:15

na Yehosadaki akachukuliwa mateka, hapo Bwana alipowachukua mateka Yuda na Yerusalemu, kwa mkono wa Nebukadreza.

1 Mambo ya Nyakati 6:16

Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari.

1 Mambo ya Nyakati 6:17

Na haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni; Libni, na Shimei.

1 Mambo ya Nyakati 6:18

Na wana wa Kohathi walikuwa Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli.

1 Mambo ya Nyakati 6:19

Wana wa Merari; Mali, na Mushi. Na hizi ndizo jamaa za Walawi, sawasawa na mbari za baba zao.

1 Mambo ya Nyakati 6:20

Wa Gershoni; mwanawe huyo ni Libni, na mwanawe huyo ni Yahathi, na mwanawe huyo ni Zima;

1 Mambo ya Nyakati 6:21

na mwanawe huyo ni Yoa, na mwanawe huyo ni Ido, na mwanawe huyo ni Zera, na mwanawe huyo ni Yeatherai.

1 Mambo ya Nyakati 6:22

Wana wa Kohathi; mwanawe huyo ni Ishari, na mwanawe huyo ni Kora, na mwanawe huyo ni Asiri;

1 Mambo ya Nyakati 6:23

na mwanawe huyo ni Elkana, na mwanawe huyo ni Ebiasafu, na mwanawe huyo ni Asiri;

1 Mambo ya Nyakati 6:24

na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Urieli, na mwanawe huyo ni Uzia, na mwanawe huyo ni Shauli.

1 Mambo ya Nyakati 6:25

Na wana wa Elkana; Amasai, na Ahimothi.

1 Mambo ya Nyakati 6:26

Kwa habari za Elkana; wana wa Elkana; mwanawe huyo ni Sufu, na mwanawe huyo ni Tohu;

1 Mambo ya Nyakati 6:27

na mwanawe huyo ni Elihu, na mwanawe huyo ni Yerohamu, na mwanawe huyo ni Elkana.

1 Mambo ya Nyakati 6:28

Na wana wa Samweli; Yoeli, mzaliwa wa kwanza, na wa pili Abia.

1 Mambo ya Nyakati 6:29

Wana wa Merari; Mali, na mwanawe huyo ni Libni, na mwanawe huyo ni Shimei, na mwanawe huyo ni Uza;

1 Mambo ya Nyakati 6:30

na mwanawe huyo ni Shimea, na mwanawe huyo ni Hagla, na mwanawe huyo ni Asaya.

1 Mambo ya Nyakati 6:31

Na hawa ndio watu aliowaweka Daudi juu ya kazi ya kuimba katika nyumba ya Bwana, sanduku lile lilipokwisha pata mahali pa kustarehe.

1 Mambo ya Nyakati 6:32

Nao wakafanya kazi yao ya kuimba mbele ya maskani ya hema ya kukutania, hata Sulemani alipokuwa amejenga ile nyumba ya Bwana huko Yerusalemu; pia wakaisimamia huduma yao sawasawa na zamu zao.

1 Mambo ya Nyakati 6:33

Na hawa ndio waliofanya huduma pamoja na wana wao. Katika wana wa Wakohathi; Hemani mwimbaji, mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli;

1 Mambo ya Nyakati 6:34

mwana wa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu;

1 Mambo ya Nyakati 6:35

mwana wa Sufu, mwana wa Elkana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai;

1 Mambo ya Nyakati 6:36

mwana wa Elkana, mwana wa Shauli, mwana wa Uzia, mwana wa Urieli;

1 Mambo ya Nyakati 6:37

mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora;

1 Mambo ya Nyakati 6:38

mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli.

1 Mambo ya Nyakati 6:39

Na nduguye Asafu, aliyesimama upande wake wa kuume, huyo Asafu alikuwa mwana wa Berekia, mwana wa Shimea;

1 Mambo ya Nyakati 6:40

mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya, mwana wa Malkiya;

1 Mambo ya Nyakati 6:41

mwana wa Yeatherai, mwana wa Zera, mwana wa Ido;

1 Mambo ya Nyakati 6:42

mwana wa Yoa, mwana wa Zima, mwana wa Shimei;

1 Mambo ya Nyakati 6:43

mwana wa Yahathi, mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi.

1 Mambo ya Nyakati 6:44

Na upande wa kushoto ndugu zao, wana wa Merari; Ethani, mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki;

1 Mambo ya Nyakati 6:45

mwana wa Hashabia, mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia;

1 Mambo ya Nyakati 6:46

mwana wa Amzi, mwana wa Bani, mwana wa Shemeri;

1 Mambo ya Nyakati 6:47

mwana wa Mali, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi.

1 Mambo ya Nyakati 6:48

Na ndugu zao, Walawi, ndio waliowekwa ili kufanya huduma yote ya maskani ya nyumba ya Mungu.

1 Mambo ya Nyakati 6:49

Lakini Haruni na wanawe ndio waliokuwa wakitoa sadaka juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya madhabahu ya kufukizia uvumba, kwa ajili ya kazi yote ya Patakatifu pa Patakatifu, ili kufanya upatanisho kwa Israeli, sawasawa na yote aliyokuwa ameyaamuru Musa, mtumishi wa Mungu.

1 Mambo ya Nyakati 6:50

Na hawa ndio wana wa Haruni; mwanawe huyo ni Eleazari, na mwanawe huyo ni Finehasi, na mwanawe huyo ni Abishua;

1 Mambo ya Nyakati 6:51

na mwanawe huyo ni Buki, na mwanawe huyo ni Uzi, na mwanawe huyo ni Serahia;

1 Mambo ya Nyakati 6:52

na mwanawe huyo ni Merayothi, na mwanawe huyo ni Amaria, na mwanawe huyo Ahitubu;

1 Mambo ya Nyakati 6:53

na mwanawe huyo ni Sadoki, na mwanawe huyo ni Ahimaasi.

1 Mambo ya Nyakati 6:54

Basi haya ndiyo makao yao, sawasawa na marago yao mipakani mwao; wana wa Haruni, katika jamaa za Wakohathi; kwani walikuwa na kura ya kwanza;

1 Mambo ya Nyakati 6:55

wakapewa Hebroni, katika nchi ya Yuda, na vijiji vyake vilivyouzunguka;

1 Mambo ya Nyakati 6:56

bali mashamba ya mji huo, na vijiji vyake, alipewa Kalebu, mwana wa Yefune.

1 Mambo ya Nyakati 6:57

Na wana wa Haruni wakapewa miji ile ya kukimbilia, nayo ni Hebroni, tena Libna pamoja na viunga vyake, na Yatiri, na Eshtemoa pamoja na viunga vyake;

1 Mambo ya Nyakati 6:58

na Holoni pamoja na viunga vyake, na Debiri pamoja na viunga vyake;

1 Mambo ya Nyakati 6:59

na Ashani pamoja na viunga vyake, na Beth-shemeshi pamoja na viunga vyake;

1 Mambo ya Nyakati 6:60

tena katika kabila ya Benyamini; Geba pamoja na viunga vyake, na Alemethi pamoja na viunga vyake, na Anathothi pamoja na viunga vyake. Miji yao yote katika jamaa zao ilikuwa miji kumi na mitatu.

1 Mambo ya Nyakati 6:61

Nao waliobaki wa wana wa Kohathi walipewa kwa kura miji kumi, katika jamaa ya kabila hiyo, yaani, nusu-kabila, nusu ya Manase.

1 Mambo ya Nyakati 6:62

Na wana wa Gershoni walipewa kwa kura miji kumi na mitatu, sawasawa na jamaa zao, katika kabila ya Isakari, na katika kabila ya Asheri, na katika kabila ya Naftali, na katika kabila ya Manase waliokaa Bashani.

1 Mambo ya Nyakati 6:63

Na wana wa Merari walipewa kwa kura miji kumi na miwili, sawasawa na jamaa zao, katika kabila ya Reubeni, na katika kabila ya Gadi, na katika kabila ya Zabuloni.

1 Mambo ya Nyakati 6:64

Na wana wa Israeli waliwapa Walawi miji hiyo pamoja na viunga vyake.

1 Mambo ya Nyakati 6:65

Tena wakawapa kwa kura miji hiyo iliyotajwa majina yake, katika kabila ya wana wa Yuda, na katika kabila ya wana wa Simeoni, na katika kabila ya wana wa Benyamini.

1 Mambo ya Nyakati 6:66

Na jamaa nyingine za wana wa Kohathi walikuwa na miji ya mipakani mwao katika kabila ya Efraimu.

1 Mambo ya Nyakati 6:67

Basi wakapewa miji ya kukimbilia, yaani, Shekemu pamoja na viunga vyake katika nchi ya milima milima ya Efraimu; na Gezeri pamoja na viunga vyake;

1 Mambo ya Nyakati 6:68

na Yokmeamu pamoja na viunga vyake, na Beth-horoni pamoja na viunga vyake;

1 Mambo ya Nyakati 6:69

na Aiyaloni pamoja na viunga vyake, na Gath-rimoni pamoja na viunga vyake;

1 Mambo ya Nyakati 6:70

na katika nusu-kabila ya Manase; Taanaki pamoja na viunga vyake, na Ibleamu pamoja na viunga vyake; kwa mabaki ya jamaa ya wana wa Kohathi.

1 Mambo ya Nyakati 6:71

Na wana wa Gershoni wakapewa, katika jamaa ya nusu-kabila ya Manase; Golani katika Bashani pamoja na viunga vyake, na Ashtarothi pamoja na viunga vyake;

1 Mambo ya Nyakati 6:72

na katika kabila ya Isakari; Kishioni pamoja na viunga vyake, na Daberathi pamoja na viunga vyake;

1 Mambo ya Nyakati 6:73

na Remethi pamoja na viunga vyake, na En-gaminu pamoja na viunga vyake;

1 Mambo ya Nyakati 6:74

na katika kabila ya Asheri; Mishali pamoja na viunga vyake, na Abdoni pamoja na viunga vyake;

1 Mambo ya Nyakati 6:75

na Helkathi pamoja na viunga vyake, na Rehobu pamoja na viunga vyake;

1 Mambo ya Nyakati 6:76

na katika kabila ya Naftali; Kedeshi katika Galilaya pamoja na viunga vyake, na Hamothi pamoja na viunga vyake, na Kiriathaimu pamoja na viunga vyake.

1 Mambo ya Nyakati 6:77

Nao mabaki ya Walawi, wana wa Merari, wakapewa, katika kabila ya Zabuloni; Rimona pamoja na viunga vyake, na Tabori pamoja na viunga vyake;

1 Mambo ya Nyakati 6:78

na ng'ambo ya mto wa Yordani huko Yeriko, upande wa mashariki wa Yordani, katika kabila ya Reubeni; Bezeri katika nyika pamoja na viunga vyake, na Yahasa pamoja na viunga vyake,

1 Mambo ya Nyakati 6:79

na Kedemothi pamoja na viunga vyake, na Mefaathi pamoja na viunga vyake;

1 Mambo ya Nyakati 6:80

na katika kabila ya Gadi; Ramothi katika Gileadi pamoja na viunga vyake, na Mahanaimu pamoja na viunga vyake;

1 Mambo ya Nyakati 6:81

na Heshboni pamoja na viunga vyake, na Yazeri pamoja na viunga vyake.