1 Mambo ya Nyakati Mlango 23 1st Chronicles

1 Mambo ya Nyakati 23:1

Basi Daudi alikuwa mzee, ameshiba siku; akamtawaza mwanawe Sulemani awe mfalme juu ya Israeli.

1 Mambo ya Nyakati 23:2

Akawakusanya wakuu wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi.

1 Mambo ya Nyakati 23:3

Nao wakahesabiwa Walawi wenye miaka thelathini na zaidi; na jumla yao kwa vichwa, mtu kwa mtu, ikapata thelathini na nane elfu.

1 Mambo ya Nyakati 23:4

Katika hao ishirini na nne elfu walikuwa wa kusimamia kazi ya nyumba ya Bwana; na sita elfu walikuwa maakida na makadhi;

1 Mambo ya Nyakati 23:5

na elfu nne walikuwa mabawabu; na elfu nne walimsifu Bwana kwa vinanda, nilivyovifanya, alisema Daudi, vya kumsifia.

1 Mambo ya Nyakati 23:6

Basi Daudi akawagawanya kuwa zamu zao sawasawa na wana wa Lawi; Gershoni, Kohathi, na Merari.

1 Mambo ya Nyakati 23:7

Wa Wagershoni; Ladani, na Shimei.

1 Mambo ya Nyakati 23:8

Wana wa Ladani; Yehieli mkuu wao, na Zethamu, na Yoeli, watu watatu.

1 Mambo ya Nyakati 23:9

Wana wa Shimei; Shelomothi, na Hazieli, na Harani, watatu. Hao walikuwa vichwa vya mbari za baba za Ladani.

1 Mambo ya Nyakati 23:10

Na wana wa Shimei; Yahathi, na Zina, na Yeushi, na Beria. Hao wanne walikuwa wana wa Shimei.

1 Mambo ya Nyakati 23:11

Naye Yahathi alikuwa mkubwa wao, na Zina alikuwa wa pili; lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; basi wakawa mbari ya baba kwa kuhesabiwa pamoja.

1 Mambo ya Nyakati 23:12

Wana wa Kohathi; Amramu, Ishari, Hebroni, na Uzieli, watu wanne.

1 Mambo ya Nyakati 23:13

Wana wa Amramu; Haruni na Musa; naye Haruni akatengwa, ili ayatakase yaliyo matakatifu sana, yeye na wanawe milele, ili kufukiza uvumba mbele za Bwana, kumtumikia, na kubariki kwa jina lake, milele.

1 Mambo ya Nyakati 23:14

Lakini kwa habari za Musa, mtu wa Mungu, wanawe hutajwa miongoni mwa kabila ya Lawi.

1 Mambo ya Nyakati 23:15

Wana wa Musa; Gershomu na Eliezeri.

1 Mambo ya Nyakati 23:16

Wana wa Gershomu; Shebueli mkuu wao.

1 Mambo ya Nyakati 23:17

Na wana wa Eliezeri; Rehabia mkuu wao. Yeye Eliezeri hakuwa na wana wengine; lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana.

1 Mambo ya Nyakati 23:18

Wana wa Ishari; Shelomithi mkuu wao.

1 Mambo ya Nyakati 23:19

Wana wa Hebroni; Yeria mkuu wao, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne.

1 Mambo ya Nyakati 23:20

Wana wa Uzieli; Mika mkuu wao, na Ishia wa pili.

1 Mambo ya Nyakati 23:21

Wana wa Merari; Mali na Mushi. Wana wa Mali; Eleazari, na Kishi.

1 Mambo ya Nyakati 23:22

Akafa Eleazari, wala hakuwa na wana, ila binti tu; na ndugu zao, wana wa Kishi, wakawaoa.

1 Mambo ya Nyakati 23:23

Wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi, watu watatu.

1 Mambo ya Nyakati 23:24

Hao walikuwa wana wa Lawi, kwa kufuata mbari za baba zao, yaani, vichwa vya mbari za baba zao waliohesabiwa, kwa hiyo hesabu ya majina yao kwa vichwa, hao walioifanya kazi ya utumishi wa nyumba ya Bwana, wenye miaka ishirini na zaidi.

1 Mambo ya Nyakati 23:25

Kwa kuwa Daudi alisema, Bwana, Mungu wa Israeli, amewastarehesha watu wake; naye hukaa Yerusalemu milele;

1 Mambo ya Nyakati 23:26

wala Walawi hawahitaji tena kuichukua maskani, na vyombo vyake vyote kwa utumishi wake.

1 Mambo ya Nyakati 23:27

Maana kwa maneno ya mwisho ya Daudi, hao wana wa Lawi walihesabiwa, wenye miaka ishirini na zaidi.

1 Mambo ya Nyakati 23:28

Kwani kazi yao ilikuwa kuwangojea wana wa Haruni katika utumishi wa nyumba ya Bwana, nyuani, na vyumbani, na kwa kuvisafisha vitakatifu vyote, ndiyo kazi ya utumishi wa nyumba ya Mungu;

1 Mambo ya Nyakati 23:29

tena kazi ya mikate ya wonyesho, na ya unga mwembamba wa sadaka ya unga; ikiwa ni wa maandazi yasiyochachwa, au wa yale yaliyotokoswa, au wa yale yaliyookwa; na kazi ya kila namna ya kipimo na cheo;

1 Mambo ya Nyakati 23:30

nao wasimame kila asubuhi kumshukuru na kumsifu Bwana, na jioni vivyo hivyo;

1 Mambo ya Nyakati 23:31

na kumtolea Bwana sadaka zote za kuteketezwa, katika siku za sabato, za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoagizwa, kwa hesabu kadiri ya agizo lake, daima mbele za Bwana;

1 Mambo ya Nyakati 23:32

tena walinde ulinzi wa hema ya kukutania, na ulinzi wa patakatifu, na ulinzi wa wana wa Haruni, ndugu zao, katika utumishi wa nyumba ya Bwana.