1 Mambo ya Nyakati Mlango 4 1st Chronicles

1 Mambo ya Nyakati 4:1

Wana wa Yuda; Peresi, na Hesroni, na Karmi, na Huri, na Shobali.

1 Mambo ya Nyakati 4:2

Na Reaya, mwana wa Shobali, akamzaa Yahathi; na Yahathi akawazaa Ahumai, na Lahadi. Hizo ndizo jamaa za Wasorathi.

1 Mambo ya Nyakati 4:3

Na hawa ndio wana wa babaye Etamu; Yezreeli, na Ishma, na Idbashi; na umbu lao aliitwa jina lake Haselelponi;

1 Mambo ya Nyakati 4:4

na Penueli, babaye Gedori, na Ezeri, babaye Husha. Hao ndio wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi, babaye Bethlehemu.

1 Mambo ya Nyakati 4:5

Naye Ashuri, babaye Tekoa, alikuwa na wake wawili, Hela na Naara.

1 Mambo ya Nyakati 4:6

Naye Naara akamzalia Ahuzamu, na Heferi, na Temeni, na Ahashtari. Hao ndio wana wa Naara.

1 Mambo ya Nyakati 4:7

Na wana wa Hela walikuwa Serethi, na Ishari, na Ethnani.

1 Mambo ya Nyakati 4:8

Na Hakosi akawazaa Anubu, na Sobeba, na jamaa za Aharheli, mwana wa Harumu.

1 Mambo ya Nyakati 4:9

Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni.

1 Mambo ya Nyakati 4:10

Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.

1 Mambo ya Nyakati 4:11

Naye Kelubu, nduguye Shuha, akamzaa Mehiri, aliyekuwa babaye Eshtoni.

1 Mambo ya Nyakati 4:12

Na Eshtoni akamzaa Beth-Rafa, na Pasea, na Tehina, babaye Ir-nahashi. Hao ni watu wa Reka.

1 Mambo ya Nyakati 4:13

Na wana wa Kenazi; Othnieli, na Seraya; na wana wa Othnieli; Hathathi.

1 Mambo ya Nyakati 4:14

Na Meonothai akamzaa Ofra; na Seraya akamzaa Yoabu, babaye bonde la Wakarashi; kwani hao walikuwa mafundi.

1 Mambo ya Nyakati 4:15

Na wana wa Kalebu, mwana wa Yefune; Iru, na Ela, na Naamu; na wana wa Ela; na Kenazi.

1 Mambo ya Nyakati 4:16

Na wana wa Yehaleleli; Zifu, na Zifa, na Tiria, na Asareli.

1 Mambo ya Nyakati 4:17

Na wana wa Ezrahi; Yetheri, na Meredi, na Eferi, na Yaloni; na Miriamu akamzalia na Shamai, na Ishba, babaye Eshtemoa.

1 Mambo ya Nyakati 4:18

Na mkewe Myahudi akawazaa Yeredi, babaye Gedori, na Heberi, babaye Soko, na Yekuthieli, babaye Zanoa. Na hawa ndio wana wa Bithia, binti Farao, ambaye Meredi alimwoa.

1 Mambo ya Nyakati 4:19

Na wana wa mkewe Hodia, umbu lake Nahamu, walikuwa babaye Keila, Mgarmi, na Eshtemoa, Mmaaka.

1 Mambo ya Nyakati 4:20

Na wana wa Shimoni; Amnoni, na Rina, na Ben-hanani, na Tiloni. Na wana wa Ishi; Zohethi, na Ben-zohethi.

1 Mambo ya Nyakati 4:21

Wana wa Shela, mwana wa Yuda; Eri, babaye Leka, na Laada, babaye Maresha, na jamaa zao wa mbari ya wafuma nguo za kitani safi, wa mbari ya Ashbea;

1 Mambo ya Nyakati 4:22

na Yokimu, na watu wa Kozeba, na Yoashi, na Sarafi waliokuwa na mamlaka katika Moabu, na Yashubi-lehemu. Na taarifa hizi ni za zamani sana.

1 Mambo ya Nyakati 4:23

Hao ndio waliokuwa wafinyanzi, na wenyeji wa Netaimu na Gedera; ndipo walipokaa pamoja na mfalme ili kufanya kazi yake.

1 Mambo ya Nyakati 4:24

Wana wa Simeoni; Yemueli, na Yamini, na Yakini, na Sohari, na Shauli;

1 Mambo ya Nyakati 4:25

na mwanawe huyo ni Shalumu, na mwanawe huyo ni Mibsamu, na mwanawe huyo ni Mishma.

1 Mambo ya Nyakati 4:26

Na wana wa Mishma; mwanawe huyo ni Hamueli, na mwanawe huyo ni Zakuri, na mwanawe huyo ni Shimei.

1 Mambo ya Nyakati 4:27

Naye Shimei alikuwa na wana wa kiume kumi na sita, na wana wa kike sita; walakini nduguze walikuwa hawana watoto wengi, tena jamaa yao yote haikuongezeka sana kwa mfano wa wana wa Yuda.

1 Mambo ya Nyakati 4:28

Nao wakakaa huko Beer-sheba, na Molada, na Hasar-shuali;

1 Mambo ya Nyakati 4:29

na huko Bilha, na Esemu, na Toladi;

1 Mambo ya Nyakati 4:30

na huko Bethueli, na Horma, na Siklagi;

1 Mambo ya Nyakati 4:31

na huko, Beth-markabothi, na Hasar-susimu, na Bethbiri, na Shaaraimu. Hiyo ndiyo miji yao hata wakati wa kumiliki Daudi.

1 Mambo ya Nyakati 4:32

Na vijiji vyao vilikuwa Etamu, na Aini, na Rimoni, na Tokeni, na Ashani, miji mitano,

1 Mambo ya Nyakati 4:33

na vijiji vyao vyote vilivyoizunguka miji iyo hiyo, mpaka Baali. Hayo ndiyo makao yao, na hati ya nasaba yao wanayo.

1 Mambo ya Nyakati 4:34

Naye Meshobabu, na Yamleki, na Yosha, mwana wa Amazia;

1 Mambo ya Nyakati 4:35

na Yoeli, na Yehu, mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli;

1 Mambo ya Nyakati 4:36

na Elioenai, na Yaakoba, na Yeshohava, na Asaya, na Adieli, na Yesimieli, na Benaya;

1 Mambo ya Nyakati 4:37

na Ziza, mwana wa Shifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya mwana wa Shimri, mwana wa Shemaya;

1 Mambo ya Nyakati 4:38

hao waliotajwa majina yao ndio waliokuwa wakuu katika jamaa zao; na mbari za baba zao zikaongezeka sana.

1 Mambo ya Nyakati 4:39

Basi wakaenda mpaka maingilio ya Gedori, naam, mpaka upande wa mashariki wa bonde hilo, ili kuwatafutia kondoo zao malisho.

1 Mambo ya Nyakati 4:40

Wakaona malisho ya unono, mazuri, na nchi yenyewe ilikuwa na nafasi, tena imetulia, na kuwa na amani; kwani waliokaa huko zamani walikuwa watu wa Hamu.

1 Mambo ya Nyakati 4:41

Na hao walioandikwa majina yao waliingia huko katika siku za Hezekia, mfalme wa Yuda, na kuzipiga hema zao, pamoja na hao Wameuni walioonekana huko, wakawaangamiza kabisa, hata siku hii ya leo, nao wakakaa huko badala yao; kwa sababu huko kulikuwa na malisho kwa kondoo zao.

1 Mambo ya Nyakati 4:42

Na baadhi yao, maana ya hao wana wa Simeoni, watu mia tano, wakaenda mpaka mlima Seiri, na majemadari wao walikuwa Pelatia, na Nearia, na Refaya, na Uzieli, wana wa Ishi.

1 Mambo ya Nyakati 4:43

Nao wakawapiga mabaki ya Waamaleki waliookoka, wakakaa huko, hata siku hii ya leo.