1 Mambo ya Nyakati 17 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Mambo ya Nyakati 17 (Swahili) 1st Chronicles 17 (English)

Ikawa, Daudi alipokuwa akikaa nyumbani mwake, Daudi akamwambia nabii Nathani, Angalia, mimi ninakaa katika nyumba ya mwerezi, bali sanduku la agano la Bwana linakaa chini ya mapazia. 1 Mambo ya Nyakati 17:1

It happened, when David lived in his house, that David said to Nathan the prophet, Behold, I dwell in a house of cedar, but the ark of the covenant of Yahweh [dwells] under curtains.

Naye Nathani akamwambia Daudi, Haya, fanya yote yaliyomo moyoni mwako; kwa maana Mungu yu pamoja nawe. 1 Mambo ya Nyakati 17:2

Nathan said to David, Do all that is in your heart; for God is with you.

Ikawa usiku uo huo, neno la Mungu likamjia Nathani, kusema, 1 Mambo ya Nyakati 17:3

It happened the same night, that the word of God came to Nathan, saying,

Nenda, kamwambie mtumishi wangu, Daudi, Bwana asema hivi, Wewe hutanijengea nyumba ya kukaa; 1 Mambo ya Nyakati 17:4

Go and tell David my servant, Thus says Yahweh, You shall not build me a house to dwell in:

kwa maana sikukaa ndani ya nyumba tangu siku ile nilipowaleta Israeli huku hata leo; lakini hema kwa hema nimehamia, na maskani kwa maskani. 1 Mambo ya Nyakati 17:5

for I have not lived in a house since the day that I brought up Israel, to this day, but have gone from tent to tent, and from [one] tent [to another].

Katika mahali mwote nilimokwenda na Israeli wote, je! Nimesema neno lo lote na mtu ye yote wa waamuzi wa Israeli, niliowaagiza kuwalisha watu wangu, nikisema, Mbona hamkunijengea nyumba ya mwerezi? 1 Mambo ya Nyakati 17:6

In all places in which I have walked with all Israel, spoke I a word with any of the judges of Israel, whom I commanded to be shepherd of my people, saying, Why have you not built me a house of cedar?

Basi sasa ndivyo utakavyomwambia mtumishi wangu Daudi, Bwana wa majeshi asema hivi, Nalikutwaa katika zizi la kondoo, katika kuwaandama kondoo ili uwe mkuu juu ya watu wangu Israeli; 1 Mambo ya Nyakati 17:7

Now therefore thus shall you tell my servant David, Thus says Yahweh of Hosts, I took you from the sheep pen, from following the sheep, that you should be prince over my people Israel:

nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina, kama jina la hao wakuu walioko duniani. 1 Mambo ya Nyakati 17:8

and I have been with you wherever you have gone, and have cut off all your enemies from before you; and I will make you a name, like the name of the great ones who are in the earth.

Tena nitawaagizia watu wangu Israeli mahali, nami nitawapanda, wapate kukaa mahali pao wenyewe, wasiondolewe tena; wala wana wa uovu hawatawatesa tena kama hapo kwanza, 1 Mambo ya Nyakati 17:9

I will appoint a place for my people Israel, and will plant them, that they may dwell in their own place, and be moved no more; neither shall the children of wickedness waste them any more, as at the first,

na tangu siku ile nilipowaamuru waamuzi wawe juu ya watu wangu Israeli, nami nitawashinda adui zako wote. Pamoja na hayo nakuambia, ya kwamba Bwana atakujengea nyumba. 1 Mambo ya Nyakati 17:10

and [as] from the day that I commanded judges to be over my people Israel; and I will subdue all your enemies. Moreover I tell you that Yahweh will build you a house.

Hata itakuwa, siku zako zitakapotimia, uende na babazo, nitainua mzao wako nyuma yako, atakayekuwa wa wana wako; nami nitaufanya imara ufalme wake. 1 Mambo ya Nyakati 17:11

It shall happen, when your days are fulfilled that you must go to be with your fathers, that I will set up your seed after you, who shall be of your sons; and I will establish his kingdom.

Yeye ndiye atakayenijengea nyumba, nami nitakifanya imara kiti cha enzi cha ufalme wake milele. 1 Mambo ya Nyakati 17:12

He shall build me a house, and I will establish his throne forever.

Nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; wala sitamwondolea fadhili zangu, kama nilivyomwondolea yeye aliyekuwa kabla yako; 1 Mambo ya Nyakati 17:13

I will be his father, and he shall be my son: and I will not take my loving kindness away from him, as I took it from him that was before you;

ila nitamstarehesha katika nyumba yangu na katika ufalme wangu milele; na kiti chake cha enzi kitathibitishwa milele. 1 Mambo ya Nyakati 17:14

but I will settle him in my house and in my kingdom forever; and his throne shall be established forever.

Kwa maneno hayo yote, na kwa maono hayo yote, ndivyo Nathani alivyonena na Daudi. 1 Mambo ya Nyakati 17:15

According to all these words, and according to all this vision, so did Nathan speak to David.

Ndipo akaingia Daudi mfalme, akaketi mbele za Bwana; akasema Mimi ni nani, Ee Bwana Mungu, na nyumba yangu ni nini, hata umenileta hata hapa? 1 Mambo ya Nyakati 17:16

Then David the king went in, and sat before Yahweh; and he said, Who am I, Yahweh God, and what is my house, that you have brought me thus far?

Tena jambo hili lilikuwa dogo machoni pako, Ee Mungu; hata umeleta habari ya nyumba yangu mimi, mtumwa wako, kwa miaka mingi inayokuja, nawe umeniangalia sawasawa na hali ya mtu mwenye cheo, Ee Bwana Mungu. 1 Mambo ya Nyakati 17:17

This was a small thing in your eyes, God; but you have spoken of your servant's house for a great while to come, and have regarded me according to the estate of a man of high degree, Yahweh God.

Na Daudi akuambie nini tena zaidi kwa habari ya heshima aliyotendewa mtumwa wako? Kwa maana wewe umemjua mtumwa wako. 1 Mambo ya Nyakati 17:18

What can David [say] yet more to you concerning the honor which is done to your servant? for you know your servant.

Ee Bwana, kwa ajili ya mtumwa wako, na kwa moyo wako mwenyewe, umeyatenda hayo makuu yote, ili yajulikane hayo matendo makuu yote. 1 Mambo ya Nyakati 17:19

Yahweh, for your servant's sake, and according to your own heart, have you worked all this greatness, to make known all [these] great things.

Ee Bwana, hakuna mwingine kama wewe, wala hakuna Mungu mwingine ila wewe, kwa kadiri tulivyosikia kwa masikio yetu. 1 Mambo ya Nyakati 17:20

Yahweh, there is none like you, neither is there any God besides you, according to all that we have heard with our ears.

Tena ni taifa lipi duniani lililo kama watu wako Israeli, ambalo Mungu alikwenda kuwakomboa kwa ajili yake mwenyewe, ili wawe watu wake, na kujifanyia jina kwa njia ya mambo makuu, yenye kuogofya, kwa kufukuza mataifa mbele ya watu wako, uliowakomboa kutoka Misri? 1 Mambo ya Nyakati 17:21

What one nation in the earth is like your people Israel, whom God went to redeem to himself for a people, to make you a name by great and awesome things, in driving out nations from before your people, whom you redeem out of Egypt?

Kwa maana watu wako Israeli ndio uliowafanya kuwa watu wako wa milele; nawe, Bwana, umekuwa Mungu wao. 1 Mambo ya Nyakati 17:22

For your people Israel did you make your own people forever; and you, Yahweh, became their God.

Basi sasa, Ee Bwana, neno lile ulilolinena katika habari za mtumwa wako, na katika habari za nyumba yake, na lifanywe imara milele, ukafanye kama ulivyosema. 1 Mambo ya Nyakati 17:23

Now, Yahweh, let the word that you have spoken concerning your servant, and concerning his house, be established forever, and do as you have spoken.

Jina lako na liwe imara, likatukuzwe milele, kusema, Bwana wa majeshi ndiye Mungu wa Israeli, naam, Mungu juu ya Israeli; na hiyo nyumba ya Daudi mtumwa wako imefanywa imara mbele zako. 1 Mambo ya Nyakati 17:24

Let your name be established and magnified forever, saying, Yahweh of Hosts is the God of Israel, even a God to Israel: and the house of David your servant is established before you.

Kwa kuwa wewe, Ee Mungu wangu, umenifunulia mimi mtumwa wako ya kuwa utanijengea nyumba; kwa hiyo mimi mtumwa wako nimeona vema moyoni mwangu kuomba mbele yako. 1 Mambo ya Nyakati 17:25

For you, my God, have revealed to your servant that you will build him a house: therefore has your servant found [in his heart] to pray before you.

Na sasa, Ee Bwana, wewe ndiwe Mungu, nawe umemwahidia mtumwa wako jambo hili jema; 1 Mambo ya Nyakati 17:26

Now, Yahweh, you are God, and have promised this good thing to your servant:

nawe sasa umekuwa radhi kuibarikia nyumba ya mtumwa wako, ipate kudumu milele mbele zako; kwa maana wewe, Bwana, umebarikia, nayo imebarikiwa milele. 1 Mambo ya Nyakati 17:27

and now it has pleased you to bless the house of your servant, that it may continue forever before you: for you, Yahweh, have blessed, and it is blessed forever.