1 Mambo ya Nyakati Mlango 26 1st Chronicles

1 Mambo ya Nyakati 26:1

Kwa zamu zao mabawabu; wa Wakora; Meshelemia mwana wa Kore, wa wana wa Ebiasafu.

1 Mambo ya Nyakati 26:2

Naye Meshelemia alikuwa na wana; Zekaria mzaliwa wa kwanza, Yediaeli wa pili, Zebadia wa tatu, Yathnieli wa nne;

1 Mambo ya Nyakati 26:3

Elamu wa tano, Yohana wa sita, Elioenai wa saba.

1 Mambo ya Nyakati 26:4

Naye Obed-edomu alikuwa na wana; Shemaya mzaliwa wa kwanza, Yehozabadi wa pili, Yoa wa tatu, na Sakari wa nne, na Nethaneli wa tano;

1 Mambo ya Nyakati 26:5

Amieli wa sita, Isakari wa saba, Peulethai wa nane; kwa jinsi Mungu alivyombariki.

1 Mambo ya Nyakati 26:6

Naye mwanawe Shemaya akazaliwa wana, waliomiliki juu ya mbari ya baba yao; kwa kuwa walikuwa waume mashujaa.

1 Mambo ya Nyakati 26:7

Wana wa Shemaya; Othni, na Refaeli, na Obedi, na Elzabadi, nduguze walikuwa mashujaa, Elihu, na Semakia.

1 Mambo ya Nyakati 26:8

Hao wote walikuwa wana wa Obed-edomu; wao na wana wao na ndugu zao, watu hodari wawezao huo utumishi; watu wa Obed-edomu sitini na wawili.

1 Mambo ya Nyakati 26:9

Naye Meshelemia alikuwa na wana na nduguze, watu mashujaa, kumi na wanane.

1 Mambo ya Nyakati 26:10

Hosa naye, wa wana wa Merari, alikuwa na wana; Shimri mkuu wao; (kwani ajapokuwa yeye si mzaliwa wa kwanza, babaye alimweka mkuu);

1 Mambo ya Nyakati 26:11

Hilkia wa pili, Tebalia wa tatu, Zekaria wa nne; wana wote wa Hosa pamoja na nduguze walikuwa watu kumi na watatu.

1 Mambo ya Nyakati 26:12

Katika hao zilikuwa zamu za mabawabu, yaani, katika hao wakuu, wenye ulinzi sawasawa na ndugu zao, wa kutumika katika nyumba ya Bwana.

1 Mambo ya Nyakati 26:13

Nao wakatupiwa kura kwa ajili ya kila lango, wadogo sawasawa na wakubwa, kwa kadiri ya mbari za baba zao.

1 Mambo ya Nyakati 26:14

Kura ya mashariki ya lango ikamwangukia Meshelemia. Ndipo wakamtupia kura Zekaria mwanawe, mshauri mwenye busara; na kura yake ikamtokea ya kaskazini.

1 Mambo ya Nyakati 26:15

Ya Obed-edomu ya kusini; na ya wanawe nyumba ya akiba.

1 Mambo ya Nyakati 26:16

Ya Shupimu na Hosa upande wa magharibi, langoni pa Shalekethi, hapo penye daraja ya kupandia, ulinzi kwa ulinzi.

1 Mambo ya Nyakati 26:17

Upande wa mashariki walikuwapo Walawi sita, kaskazini wanne kila siku, kusini wanne kila siku, na wa nyumba ya akiba wawili wawili.

1 Mambo ya Nyakati 26:18

Penye Parbari upande wa magharibi, walikuwapo wanne darajani, na wawili huko Parbari.

1 Mambo ya Nyakati 26:19

Hizo ndizo zamu za mabawabu; wa wana wa Wakora, na wa wana wa Merari.

1 Mambo ya Nyakati 26:20

Na katika Walawi; Ahia alikuwa juu ya hazina za nyumba ya Mungu, na juu ya hazina za vitu vilivyowekwa wakfu.

1 Mambo ya Nyakati 26:21

Wana wa Ladani; wana wa Wagershoni waliokuwa wa Ladani; wakuu wa mbari za mababa waliokuwa wa Ladani, Mgershoni; Yehieli.

1 Mambo ya Nyakati 26:22

Wana wa Yehieli; Zethamu, na Yoeli nduguye, juu ya hazina za nyumba ya Bwana.

1 Mambo ya Nyakati 26:23

Wa Waamramu, wa Waishari, wa Wahebroni, wa Wauzieli;

1 Mambo ya Nyakati 26:24

na Shebueli, mwana wa Gershomu, mwana wa Musa, alikuwa mtawala hazina zote.

1 Mambo ya Nyakati 26:25

Na nduguze; wa Eliezeri, Rehabia mwanawe, na Ishia mwanawe, na Yoramu mwanawe, na Zikri mwanawe, na Shelomothi mwanawe.

1 Mambo ya Nyakati 26:26

Huyo Shelomothi na ndugu zake walikuwa juu ya hazina zote za vitu vilivyowekwa wakfu, alivyoviweka wakfu mfalme Daudi, na hao wakuu wa mbari za mababa, na maakida wa maelfu na wa mamia, na maakida wa jeshi.

1 Mambo ya Nyakati 26:27

Katika nyara zilizopatikana vitani, waliweka wakfu sehemu, ili kuitengeneza nyumba ya Bwana.

1 Mambo ya Nyakati 26:28

Na vyote alivyoviweka wakfu Samweli mwonaji, na Sauli mwana wa Kishi, na Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Seruya; na mtu ye yote aliyekiweka wakfu kitu cho chote, kilikuwa chini ya mkono wa Shelomothi na nduguze.

1 Mambo ya Nyakati 26:29

Katika Waishari, Kenania na wanawe walikuwa kwa ajili ya kazi ya nje juu ya Israeli, kuwa maakida na makadhi.

1 Mambo ya Nyakati 26:30

Katika Wahebroni, Hashabia na nduguze, mashujaa, elfu na mia saba, walikuwa na usimamizi juu ya Israeli ng'ambo ya Yordani upande wa magharibi; kwa ajili ya kazi zote za Bwana, na kwa utumishi wa mfalme.

1 Mambo ya Nyakati 26:31

Katika Wahebroni Yeria alikuwa mkuu, yaani, wa hao Wahebroni kwa kufuata vizazi vyao kwa mbari za mababa. Katika mwaka arobaini wa kutawala kwake Daudi wakatafutwa, wakaonekana huko Yazeri ya Gileadi miongoni mwao waume mashujaa.

1 Mambo ya Nyakati 26:32

Na nduguze, mashujaa, walikuwa elfu mbili na mia saba, wakuu wa mbari za mababa, ambao mfalme Daudi aliwaweka wawe wasimamizi juu ya Wareubeni, na Wagadi, na nusu kabila ya Wamanase, kwa ajili ya kila neno lililomhusu Mungu, na kwa mambo ya mfalme.